Thursday, November 26, 2009

URAFIKI WA MASHAKA...


Hawa jamaa walikutwa leo na Kamera yangu wakiwa katika mshikamano wa aina yake katika kituo cha Mabasi cha Ubungo jijini hapa... Hawa ni Masai na Mzungu...

TCC MLIPAKODI WA MWAKA

Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), leo mchana imekabidhiwa tuzo ya mlipakodi wa mwaka toka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, wakati wa maadhimisho ya nne ya mlipakodi nchini yaliyofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini hapa.

Mshindi wa kwanza wa ulipajikodi wa mwaka, mwakilishi wa TCC (kushoto) na Mshindi wa tatu mwakilishi wa benki ya CRDB wakiwa katika pozi

Mjomba 'mrisho mpoto' naye alikuwepo katika upande wa burudani...

Sunday, November 22, 2009

CHADEMA YAANZA KUPANGUKA TARATIIBU


Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi Taifa, James Mbatia akikabidhi kadi ya uanachama kwa mwanachama mpya ambaye awali alikuwa Ofisa Habari wa CHADEMA, DAvid KAfulila leo katika makao makuu ya chama hicho, Ilala Dar es Salaam

KARUME AANZA KAMPENI MAPEMA VISIWANI...


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume akipokea maandamano ya wananchi na wanachama wa Chama cha MapinduziCCM wa Mikoa Mitano ya Unguja, yaliyofanyika katika uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti Mkoa wa Mjini Magharibi jana.

SHOPPING INAENDELEA KAMA KAWAIDA MLIMANI CITY

Tamasha la 'Mlimani City Shopping Carnival' lililofunguliwa Ijumaa iliyopita katika viwanja vya Mlimani city, limeingia siku yake ya tatu leo.

Lengo la tamasha hilo ni kuwashawishi watanzania kujenga utamaduni wa kufanya shopping katika maduka makubwa na kuondoa dhana tofauti iliyojengeka miongoni mwao kwamba shopping katika maduka hayo 'Malls' 'Plazas' na hata Supermarkets hufanywa na watu weupe pekee...

Baadhi ya wajasiriamali wakiendelea kuuza bidhaa zao katika tamasha hilo leo mchana..

UBABE UNAPOHAMIA BARABARANI...

ELIMU YA AJABU NDANI YA MSITU

Unaweza ukastaajabu lakini ni kweli... Hili ni tukio la aina yake ambalo wengi wetu tumekuwa tukisikia tu kupitia vyombo mbalimbali vya habari na kadhalika... Katika hali isiyo ya kawaida Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya amewakuta watoto wadogo wakazi wa Kijiji cha Igumbiro, Tarafa ya Lupiro, Wilayani Ulanga zaidi ya kilometa 12 toka kijijini mwishoni mwa wiki wakifundishwa kusoma, kuandika, kuhesabu na kujua lugha ya kiswahili ndani ya Msitu wa hifadhi ya asili wa Nanji.

Watoto hao walikuwa wakifundishwa na mwalimu asiye rasmi aliyetambulika kwa jina la Msuya Shaaban.


Watoto hao wakiwa na mwalimu wao msituni...

Tuesday, November 17, 2009

WALIMU WA PRIMARY WENYE DIGRII ZAO KUPEWA SHAVU

Serikali imesema itatoa 'shavu' kwa walimu wa Primary wenye digrii zao kufundisha katika shule za Sekondari. Katibu Mkuu Kiongozi wa nchi, Philemon Luhanjo ameyasema hayo leo alipofanya mkutano na wadau wa mambo ya habari jijini hapa.


Katibu Mkuu kiongozi, Philemon Luhanjo akizungumza leo na waandishi wa habari

Monday, November 16, 2009

ANNE KILANGO AMWAGA MACHOZI SAME

Safari ilianza hivi:


Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela alianza safari yake ya kupanda mlima kuelekea kwenye maafa akisaidiwa na Mbunge wa Vunjo, Alloyce Kimaro (kulia).


Bada ya kushuhudia maafa hayo, Mbunge huyu alishindwa kujizuia na kuanza kuangua kilio hadharani... Lakini wamama wa kijijini pale walimfariji...


Hapa akina mama hawa wa kijijini hapo wakiendelea kumfariji Mama Anna kilango..


Baada ya hapo Mama Anne Kilango alimshukuru Mungu na kumuomba awalaze marehemu wote mahala pema peponi kama anavyoonekana...

Maporomoko ya Miamba yaliyotokea wiki iliyopita katika Kijiji cha Goha, Wilayani Same na kusababisha vifo vya watu 24 mpaka kufikia jana. Pia mali mbalimbali za wanakijiji hao ziliharibika ikiwamo mazao ya shambani, mifugo na kadhalika...

Mungu azilaze roho za Marehemu hao mahala pema peponi.

Saturday, November 14, 2009

Hivi ndivyo Mamba Myamba, Same ilivyoporomoka...







NB: Picha zote zinaonyesha harakati za ufukuaji miili ya marehemu waliofukiwa na miamba katika kijiji cha Goha, Mamba Myamba, Same mkoani Kilimanjaro kama zilivyopigwa na mdau wetu

Friday, November 13, 2009

MAHUJAJI WAKWAMA UWANJA WA NDEGE DAR

Zaidi ya Mahujaji 35 waliokuwa wasafiri kuelekea Makka kwa ajili ya Ibada ya Hijja wamekwama leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Sababu ya kukwama kwao ni kushindwa kufikia makubaliano yao na wakala wa ndege wa Kampuni ya Skylink ambao ndio waliokuwa wakishughulikia masuala yao ya safari.

HALMASHAURI ZA MIJI ZAKABIDHIWA MAGARI, PIKIPIKI NA PRINTERS

Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na wahisani wamekabidhi magari 57 aina ya Nissan Patrol, Pikipiki 407 pamoja na printers 286 kwa Halmashauri za miji Midogo, ofisi za Mabonde na ofisi za Wizara kwa ajili ya kusaidia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP), leo jijini hapa Dar es Salaam.


sehemu ya pikipiki 407 zilizotolewa na wizara

sehemu ya magari 57 yaliyokabidhiwa

Monday, November 2, 2009

SOMA HIYO KARATASI KWA MAKINI... OLE WAKO UKUTWE UKI... UTAWAJUA MGAMBO...

JK aipa changamoto Sekta ya Afya

Rais Jakaya Kikwete leo amefungua rasmi shule ya meno ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Tiba na Afya Muhimbili (MUHAS, jijini ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali yake ya kuboresha sekta ya Afya kwa nyanja zote.

Mbali na shule hiyo, pia Rais Kikwete alifungua huduma mbalimbali zitakazoanza kutolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zikiwemo matibabu ya figo na nyinginezo.

Rais Kikwete amesema Serikali yake imedhamiria kuboresha afya za wananchi kwa kuhakikisha inatoa fungu kubwa la fedha kugharamia zahanati za vijijini, kata na hospitali za wilaya.

"Afya za wananchi zikiwa bora, na maisha yao yatakuwa bora. Kila mtanzania apate huduma ya afya, tujenge vituo vya afya, zahanati karibu na wananchi." Alisema leo.

Rais Jakaya Kikwete, wadau wa afya na wataalamu mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na mashine ya kupima figo leo mchana Muhimbili