Tuesday, March 20, 2012

JK AZINDUA MWAKA WA KIMATAIFA WA USHIRIKA, AZINDUA UJENZI WA JENGO LA USHIRIKA


Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Jengo la Ushirika la ghorofa 20. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza (kushoto) na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika nchini (TFC), Hussein Wakasuvi.


Rais Jakaya Kikwete akipewa maelezo na Mkandarasi Mkuu wa ujenzi wa jengo la Ushirika lenye ghorofa 20, Wang Xiangdong wa kampuni ya ujenzi ya kichina (CCECC) inayojenga jengo hilo.

Sehemu ya wafanyakazi wa TFC na Maofisa wengine wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete


Rais Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Mwaka wa Kimataifa wa Ushirika, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.


Rais Jakaya Kikwete akipewa maelezo kuhusu miradi mabalimbali inayotekelezwa na wanachama wa Chama cha kuweka na kukopa cha Bandarini Saccos na Mwenyekiti wa chama hicho, Stella Mutayabarwa wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Kimataifa wa Saccos, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.


Rais Jakaya Kikwete akitazama bidhaa zinazotengenezwa na wanachama wa Chama cha Kuweka na kukopa cha ORWIDO Saccos.


Rais Jakaya Kikwete akitazama bidhaa za nafaka zinazozalishwa na wanachama wa Chama cha kuweka na kukopa cha WANAMA.


Mzuka wa ngoma unapopanda. Msanii wa ngoma akicheza kwa hisia wakati wa sherehe hizo.

GURUMO ANAENDELEA VIZURI


Msanii Mkongwe wa bendi Kongwe ya Msondo Ngoma Music, Muhidini Gurumo akiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es salaam akipimwa mapigo ya Moyo na Ofisa Muuguzi Msaidizi wa Hospital hiyo, Suraiya Mohamed alipolazwa kufanyiwa uchunguzi wa kina toka mwishoni mwa wiki iliyopita

source: www.burudan.blogspot.com

DK SHEIN AKUTANA NA VIONGOZI WA WAFANYABIASHARA NA WAKULIMA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizunagumza na Uongozi wa Baraza la Wafanyabiashara, Wenye viwanda na Wakulima Zanzibar walipofika ikulu Mjini Zanzibar jana na walizungumzia masuala ya ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta za Umma,(wa tatu kulia)ni Rais wa Jumuiya ya wafanya Biashara na wenyeviwanda na wakulima,(Chamber) Mbarouk Omar.

source: Zanzibar State House

SIOI SUMARI AENDELEZA MOTO WA KAMPENI ZAKE ARUMERU


Sioi akisalimiana na wananchi alipowasili kwenye mkutano wa Olkung'wado kata ya Ngarenanyuki.


Sioi akiaalimia vijana kijiji cha Uwiro, Ngarenanyuki.


Kina mama wa Olkung'wado kata ya Ngarenanyuki wakimshangilia mgombea wa CCM, Sioi

LOWASSA AHUDHURIA SHEREHE ZA KUSIMIKWA ASKOFU MKUU MPYA WA JIMBO LA IFAKARA



Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel bendera kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo, Salitaris Libena zilizofanyika jana Ifakara, Mkoani Morogoro.


Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kwenye sherehe za uzinduzi wa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo, Salitaris Libena zilizofanyika jana Ifakara, Mkoani Morogoro.


Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara,Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa Viongozi wa Serikali waliohudhulia Sherehe hizo za kusimikwa kwake jana.



Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa salamu kwa wakristo waliofika kwenye Sherehe hizo leo,ambapo ameliomba Kanisa Katoliki kuisaidia serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.


Mh. Lowassa akiwapungia mkono wakazi wa Ifakara.


Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo mara baada ya kumalizika kwa Sherehe ya Kuzindua Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo iliyofanyika leo Ifakara,Mkoani Morogoro.

Monday, March 19, 2012

MWAKYEMBE AANZA MZIGO RASMI, ASEMA YUKO FITI


Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwasili Ofisini kwake leo asubuhi kwa kuanza rasmi kazi.

SHEREHE ZA MIAKA 10 YA NHIF ZAFANA DAR


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akionesha kitabu chenye ripoti ya hali ya afya kwa vijijini baada ya kukizindua wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo, Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), deogratias Ntukamazina.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu, Frederick Sumaye.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii (awamu ya tatu), Anna Abdallah.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (awamu ya tatu), Willison Mukama.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa Margaret Sitta.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Faraja Kihongole.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo, Beda Msimbe.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa mwandishi wa habari wa the Guardian, Joyce Bazira.


Waandishi mbalimbali wa habari wakionesha kitabu chenye ripoti ya hali ya afya vijijini baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipokea zawadi maalumu kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Deogratias Ntukamazina.


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa mwandishi, Muhidini Michuzi.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii 9awamu ya tatu), Dk Hussein Mwinyi. Wanaoshuhudia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye.

SAMIA SULUHU AKUTANA NA VIONGOZI WA WALEMAVU WA MACHO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan akizungumza na vingozi wa Chama cha Walemavu wa Macho nchini wakati walipomtembelea Ofisini Kwake Mtaa wa Luthuli Mjini Dar es Salaam leo. (Picha na Ali Meja)

CHUPUCHUPU...



Mkazi wa Dar es Salaam ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akipepewa baada ya kuzimia kutokana na ajali iliyohusisha daladala lenye namba za usajili T 861BDH inayofanya safari zake kati ya Kisarawe na Buguruni na gari jingine aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 238 BSF, eneo la Kisumu, Pugu, jijini juzi. Hakuna aliyejeruhiwa katika ajali hiyo. (Picha na Fadhili Akida)


Mtoto akimwangalia Mama yake ambaye jina lake halikufahamika mara moja baada ya kuanguka ghafla na kupoteza fahamu kutokana na ajali iliyohusisha daladala alilokuwa amepanda na gari jingine aina ya Toyota Hilux, eneo la Kisumu, Pugu, Dar es Salaam jana jioni. Hakuna aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.


Wasamari wakiwa wamembeba Mama huyo kumuingiza kwenye gari kwa ajili ya kumpeleka hospitali.

KAMPENI ZA UDIWANI SONGEA, MWANZA ZAPAMBA MOTO


Mwenyekiti wa chadema Mkoani Ruvuma Joseph Fuime akizungumza jana wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani katika kata ya Lizaboni manispaa ya Songea.


Wafuasi wa chadema mjjini Songea wakimsikiliza mbunge wa chama hicho Chiku Abwao hayupo pichani, jana wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani katika kata ya Londoni mjini Songea.


Mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kata ya Lizabon Alanus Mwanja Mlongo, akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika viwanja vya Londoni mjini Songea.


Mbunge wa viti maalumCHADEMA mh Chiku Abwao akizungumza jana wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya London mjini Songea.

LOWASSA ATEMBELEA SHULE YA ST. ANNE MOROGORO


Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro, Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.


Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro, Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.


Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.


Wanafunzi wa Shule ya Sekindari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Mh. Waziri Mkuu Mstaafu.


Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.

Friday, February 24, 2012

SUMBAWANGA YAZINDUA KAMPENI YA USAFI ‘SUMBAWANGA NG’ARA’


MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya akimwongoza Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal katika eneo la mkutano wa hadhara mjini Sumbawanga ambapo alisalimiana na wananchi na badaye alizindua kampeni ya kuuweka safi mji wa Sumbawanga iitwayo 'Sumbawanga ng'ara".


Mama Asha Bilal akimsalimia mtoto Juma Kapele(08) mlemavu wa ngozi 'albino' alipotembelea kituo cha kulelea watotot yatima kinachomilikiwa na kanisa katoliki cha Mtakatifu Martin de Pore kilichpo katika eneo la Katandala mjini Sumbawanga, mtoto Juma alipokelewa mawaka jana na kituo hicho baada ya kutoroshwa na mtu ikidaiwa kwa imani za kishirikina ambapo baada ya siku tatu aliokotwa porini akiwa ametelekezwa lakini alikuwa amepingwa chale mwili mzima


MKuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya akimkabidhi vifaa vya usafi Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal ili naye awakabidhi kikundi kinachofanya usafi katika mjini huo wa Sumbawanga muda mfupi kabla dk Bilal hajazindua kampeni ya usafi maarufu kama "Sumbawanga ng'ara"

source: Peti Siyame