Wednesday, March 31, 2010

KAMPENI ZAANZA RASMI: BATISTA ATANGAZA KUMN'GOA CHAMI JIMBO LA MOSHI VIJINI

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Moshi, Batista Kiteve ametangaza nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Moshi Vijijini katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Batista alitangaza azma yake hiyo leo jijini hapa alipofanya mkutano na waandishi wa habari. Kwa sasa jimbo hilo linashikiliwa na Cyril Chami.


BATISTA

TATIANA KUFANYA BIRTHDAY PARTY YAKE JIJINI

Aliyekuwa mwakilishi wa Shindano la Big Brother Africa-2, Tatiana Durao raia wa Angola, anatarajia kuangusha boonge la party jijini hapa Aprili 8.

Tatiana ambaye umaarufu wake umekuja baada ya muda mwingi kuonekana kuwa karibu sana na mshiriki toka Tanzania, Richard Bezuidenhot 'Richie' katika shindano hilo mpaka wengi kuvuta hisia kuwa wana uhusiano wa kimapenzi, alikuwa akifanya mazungumzo na wandishi wa habari leo jijini.

Amesema baada ya party yake hiyo atasafiri kwenda visiwa vya Zanzibar


Tatiana

Tuesday, March 30, 2010

MPENDAZOE KUJITOA CCM


Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kufanya mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kutangaza azma yake ya kujitoa Chama ha Mapinduzi (CCM) leo mchana

MKUTANO MKUBWA WA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI KUFANYIKA MEI 3 NA 4


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji Afrika (ICF), Omari Issa (wa pili kushoto) akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana Dar es Salaam kuhusu kufanyika kwa mkutano mkubwa wa Mazingira ya Uwekezaji unaotarajiwa kufanyika Mei 3 na 4 mwaka huu. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi wa tathmini na usimamizi wa mradi, Chimere Diop, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa mfuko huo, Emilienne Macauley na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mradi, Martin Schubert.

MPANGO MPYA WA UZAZI WA MPANGO WAZINDULIWA LEO


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa akikata utepe kuzindua rasimu ya mpango wa taifa uliokasimiwa kwa uzazi wa mpango (NFPCIP) leo jijini hapa


Mrisho Mpoto na waimbaji wa Mjomba band wakilishambulia jukwaa wakati wa uzinduzi huo

Monday, March 29, 2010

SIR ERIKSSON BOSI MPYA IVORY COAST

Bosi wa zamani wa timu ya Taifa ya England, Sven Goran Eriksson ataanza kuonekana katika michuano ya Kombe la Dunia msimu huu akiwa na timu ya taifa ya Ivory Coast.




Sven Goran Eriksson

30 WAUAWA KWA MABOMU YA KUJITOA MUHANGA MOSCOW

Watu 37 wamekufa na wengine kujeruhiwa baada ya wanawake wawili kujitoa muhanga.

Mamlaka za Urusi zimesema kuwa majeshi ya nchi hiyo kaskaini mwa Caucasus yalikuwa yakiendesha mapigano na majeshi ya uasi.

Rais wa Urusi, Dmitri Medvedev ametoa salamu za rambirambi na kusema kuwa nchi yake itapigana na magaidi pasipo kusita mpaka kieleweke.

"I will fight terrorism without hesitation and to the end"


MADEREVA TABATA WATAKA UHURU WA KUTANUA NA KUCHOMEKEANA...

Katika hali ya kushangaza wengi, madereva wa daladala wanaofanya kazi zao kati ya Tabata na maeneo mengine ya jiji hili leo wameendesha mgomo wa takribani saa nne wakishinikiza kupewa uhuru wa kuchomekea, kutanua na kutovaa sare.



Sponsor ilifika eneo la tukio majira ya sa tatu asubuhi na kukuta msongamano mkubwa wa abiria vituoni wakisubiri usafiri wa daladala bila ya mafanikio yoyote, huku wengine wakiwa wamekata tamaa ya kupata usafiri huo.

Waliiambia sponsor kuwa hawajui kwa nini maderev hao wamegoma maana hakukuwa na taarifa rasmi iliyotolewa kupitia vyombo husika ikiwemo chama chao cha madereva. "Nimefika hapa tangu saa 2 lakini ndo kama unavyoona hivi ndugu yangu hakuna daladala." Alisema mkazi mmoja wa Tabata Bima.



Mmoja wa wafanyakazi wa daladala hizo aliyekata kutaja jina lake aliiambia Sponsor kuwa askari wa usalama barabarani maarufu 'wazee wa feva' wanawabana sana na kushindwa kufikia malengo yao na hivyo kuona suluhu ni kugoma.

"Mfano unakuta kuna foleni, sasa ukifungua mlango ili watu wapate hewa ndani, askari anakupiga bao. Ukichomekea au kutanua kutokana na foleni ya pale kwa ali hamza unapigwa bao." Alisema.

Friday, March 26, 2010

AJALI YA KIBAMBA: MAMA MJAMZITO, BABA NA MTOTO WAFA, NI SIMANZI MITAA YA KIBAMBA

Katika hali ya kusikitisha imebainika kuwa Baba, Mama na Mtoto ni miongoni mwa waliokufa katika ajali ya gari iliyotokea Kibamba Darajani, Dar es Salaam jana.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Sponsor leo katika mitaa mbalimbali ya Kibamba, imebainika kuwa marehemu Ibrahim Hussein na mke wake Zainab Ally ambaye alikuwa ni mjamzito walikufa papo hapo katika ajali hiyo wakiwa njiani kuelekea hospitali.

Mdogo wa Marehemu Zainab, Sharifa Ally ameiambia Sponsor kuwa marehemu hao mume na mke wake ambaye alikuwa ni mjamzito iliwalazimu kuondoka mapema alfajiri kuelekea hospitali ili kuepuka misururu ya magari iliyozoeleka katika barabara ya Morogoro, lakini hawakufikia malengo yao na ndipo umauti ulipowakuta njiani, meta chache sana kutoka walipopandia daladala. Marehemu Zainab alikuwa katika hatua za mwisho za kujifungua.

Katika ajali hiyo ya kusikitisha, ujauzito wa marehemu Zainab uliharibika vibaya palepale na mtoto kutoka nje kwa bahati mbaya. Kwa maana nyingine tunaweza kusema, marehemu Zainab alijifungua kwa lazima na tena kwa njia isiyo halali.

Miili ya marehemu hao wote watatu inatarajiwa kuzikwa jioni hii katika makabauri yaliyopo jirani na nyumbani kwao, Kibamba Dar es Salaam. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.


Mtoto Mwanaidi Ibrahimu, yatima aliyeachwa na wazazi wake wawili

Katika hatua nyingine, Sponsor imeshuhudia simanzi iliyotawala katika mitaa mbalimbali ya Kibamba CCM ambako asilimia kubwa ya abiria waliokufa katika ajali ile waliokuwa wakiishi huko.

Haikuwa rahisi kutoona vikundi vya watu vikijadili hili na lile kuhusiana na tukio lile la ajali ya Kibamba.

Nyumbani kwa Mzee Hussein, ambaye kijana wake ndie aliyekuwa kondakta wa daladala lile napo vilio na simanzi vilitawala.

"Tunasafirisha leo kwenda kuzika kwa Ngwandu, Tanga." Alisema mzee Hussein.


Ndugu wa karibu wakiomboleza msiba wa marehemu Shukuru Hussein, aliyekuwa kondakta wa daladala iliyopata ajali

Thursday, March 25, 2010

10 WAFA PAPO HAPO KATIKA AJALI MBAYA KIBAMBA

Watu 10 wamekufa papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi dogo la abiria na lori la mafuta, Kibamba darajani, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Sponsor ilifika eneo la tukio na kushuhudia askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji, wanajeshi na raia wakiopoa miili ya maiti zilizokuwa zimekwama katika basi hilo.

Kwa mujibu walioshuhudia ajali hiyo wamesema ilitokea majira ya saa 11 alfajiri wakati lori la kubeba mafuta maarufu 'tanker' lililokuwa likitokea Ubungo kujaribu ku'overtake' gari jingine na hivyo kukutana uso kwa uso na daladala hiyo iliyokuwa ikitokea Kibamba kuelekea Ubungo kabla ya kuburuzana hadi mtaroni na kulaliwa na lori hilo.

Sponsor ilishuhudia daladala hilo likiwa lime'banda' na kuwa mithili ya chapati huku miili ya watu iliyokuwa nayo imechanwa vibaya na mingine kutumbuka hadi utumbo kutoka nje ikiwa ndani yake.

Hili ni tukio la pili la aina yake katika kipindi cha miaka mitatu ukiachana na tukio jingine la aina hii lililowahi kutokea Kimara miaka mitatu iliyopta.

Hadi Sponsor inakwenda mitamboni bado zoezi la kuopoa miili hiyo lilikuwa linaendelea.

PICHA ZA TUKIO:


CHINA YAMWAGA PIKIPIKI 100 DAR CITY



Halmashauri ya Jiji la Changzho, China imetoa msaada wa pikipiki 100 kwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia maendeleo katika kata zake.

Meya wa jiji hilo Weng Wengcheng amesema msaada huo ni matunda ya ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo mbili hususan miji hii miwili ya Changzhou na Dar es Salaam.

Miji hiyo ni miji dada kutokana na ushirikiano wa kiuchumi uliopo kati yao.

Monday, March 22, 2010

MVUA, WATOTO NA HATARI BARABARANI



Nimegundua kuwa watoto wenye umri mdogo hasa wale walio darasa la kwanza, hupenda kucheza katika mvua pindi zinaponyesha.

Katika pitapita zangu za kutafuta habari leo asubuhi nikianzia wilayani Kinondoni, Ilala na kumalizia Temeke nimekutana na watoto ambao ni wanafunzi katika shule mbalimbali za wilaya hizo wakiwa vifua wazi huku wakikimbizana katikati ya mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha kwa mafungu jijini hapa.

Nilipigwa butwaa nilipowaona watoto wakikatiza barabara ya Kawawa eneo la Kigogo, wakikimbia pasipo kuangalia usalama wao huku magari yaendayo kasi yakipishana nao.

Hali hiyo ilinistaajabisha na kutafakari kuhusu umuhimu wa wazazi kuchukua tahadhari kwa watoto wao pindi mvua zinaponyesha.

UANDIKISHAJI WAPIGAKURA WAANZA LEO DAR



Zoezi la kuboresha daftari la wapigakura limeanza leo katika vituo mbalimbali vilivyoteuliwa, jijini hapa leo.

Sponsor ilishuhudia maeneo mbalimbali hasa katika shule za msingi kukiwa na mikusanyiko ya wananchi wakijiandikisha katika daftari la wapigakura.

Vituo hivyo ni Hananasif Kinondoni, Basata Ilala na Shule ya Msingi Makamba Temeke.

"Kwa ujumla zoezi limeanza vizuri, wananchi wameitikia wito." Alisema Flora Luhamo, mwandikishaji wa kituo cha Hananasif.

Monday, March 15, 2010

HUU NI UCHIZI AU KUJIENDEKEZA?



Mkazi huyu wa jijini hapa amekutwa na blog hii akikoga maji machafu yanayotoa harufu kali, eneo la Tandika Transfoma jana jioni. Haikufahamika mara moja kama jamaa huyu ni mgonjwa wa akili ama anajiendekeza tu.

Lakini sidhani kama mgonjwa wa akili hukumbuka hata kukoga maji.

Kwa mpango huo basi, hii ni hatari kwa afya yake jamaa huyu.

JK AAPISHA MAKATIBU WATENDAJI TUME YA MIPANGO

Rais Jakaya Kikwete leo amewaapisha Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, pamoja na Manaibu Katibu watendaji wanne, Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Kikwete amemwapisha ndugu Dk. Phillip Isidori Mpango kuwa Katibu Mtendaji wa Tue ya Mipango, Bw. Maduka Paul Kessy kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa tume hiyo pamoja na Bi. Happiness Ngoti Mgalula naye pia kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa tume hiyo.



Wengine ni Bi. Florence Mwanri ambaye ni Naibu Katibu wa Tume hiyo ya Mipango na Bw. Clifford Katondo Tandali naye pia kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo.

Hafla ya kuwaapisha Katibu na Manaibu Katibu wake imefanyika Ikulu, jijini Dar es Salam leo asubuhi.

Friday, March 12, 2010

A NEW DAY HAS COME...

Nine Months have passed, leaving a newly borned baby boy. He's a son of mine. Surely, I'm now joined a wonderful world. The World of a Families.

I'm now called a dadii, compare to the past days. I'm really proud of it! Thank you God for bring me my Lovely SON!

Friday, March 5, 2010

MUHIMBILI SACCOS YAMWAGA VYANDARUA KWA WAGONJWA

Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) kwa wafanyakazi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo kimetoa msaada wa vyandarua 100 vyenye thamani ya sh 580,000/ kwa Mama na Watoto katika hospitali ya Muhimbili.

Msaada huo umekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza Kampeni ya Zinduka, inayopiga Vita Ugonjwa wa Malaria.


Mwenyekiti wa SACCOS hiyo (kushoto) akikabidhi vyandarua hivyo

WABONGO WAFUNZWA KUTUMIA 'FALK LIFT'

Kampuni ya SURVE Consultant Ltd, leo imefunga mafunzo yake ya wiki 3 kwa wahitimu 18 wa mafunzo ya utumiaji salama wa 'Falk Lifts'. Falk Lift ni magari maalumu ya kubebea mizigo mizito kutoka eneo moja kwenda jingine.

Mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika katika Kampuni ya MANTRAC-TANZANIA ambao ni Wakala wa Kampuni ya CATERPILLAR.


Wahitimu wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja

Thursday, March 4, 2010

GREAT LAKES MEET ON HIV/AIDS INITIATIVES

Great Lakes Country Members met today morning to discus issues concerning HIV/AIDS new epidemic.

Vice President, Dr. Ali Mohammed Shein officiate the 3-day Meeting at the Whitesands Hotel, in the City.

Kenya, Uganda, DR-Congo, Rwanda and Burundi are the Countries participate the Meeting.


Vice President, Dr Shein (c), Health and Social Welfare Minister, Prof. Mwakyusa (R) and Philip Marmo of Parliametary Affairs


Vice President, Dr Shein (c) in a group picture with delegates