Monday, March 29, 2010

MADEREVA TABATA WATAKA UHURU WA KUTANUA NA KUCHOMEKEANA...

Katika hali ya kushangaza wengi, madereva wa daladala wanaofanya kazi zao kati ya Tabata na maeneo mengine ya jiji hili leo wameendesha mgomo wa takribani saa nne wakishinikiza kupewa uhuru wa kuchomekea, kutanua na kutovaa sare.



Sponsor ilifika eneo la tukio majira ya sa tatu asubuhi na kukuta msongamano mkubwa wa abiria vituoni wakisubiri usafiri wa daladala bila ya mafanikio yoyote, huku wengine wakiwa wamekata tamaa ya kupata usafiri huo.

Waliiambia sponsor kuwa hawajui kwa nini maderev hao wamegoma maana hakukuwa na taarifa rasmi iliyotolewa kupitia vyombo husika ikiwemo chama chao cha madereva. "Nimefika hapa tangu saa 2 lakini ndo kama unavyoona hivi ndugu yangu hakuna daladala." Alisema mkazi mmoja wa Tabata Bima.



Mmoja wa wafanyakazi wa daladala hizo aliyekata kutaja jina lake aliiambia Sponsor kuwa askari wa usalama barabarani maarufu 'wazee wa feva' wanawabana sana na kushindwa kufikia malengo yao na hivyo kuona suluhu ni kugoma.

"Mfano unakuta kuna foleni, sasa ukifungua mlango ili watu wapate hewa ndani, askari anakupiga bao. Ukichomekea au kutanua kutokana na foleni ya pale kwa ali hamza unapigwa bao." Alisema.

No comments:

Post a Comment