Thursday, March 25, 2010

10 WAFA PAPO HAPO KATIKA AJALI MBAYA KIBAMBA

Watu 10 wamekufa papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi dogo la abiria na lori la mafuta, Kibamba darajani, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Sponsor ilifika eneo la tukio na kushuhudia askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji, wanajeshi na raia wakiopoa miili ya maiti zilizokuwa zimekwama katika basi hilo.

Kwa mujibu walioshuhudia ajali hiyo wamesema ilitokea majira ya saa 11 alfajiri wakati lori la kubeba mafuta maarufu 'tanker' lililokuwa likitokea Ubungo kujaribu ku'overtake' gari jingine na hivyo kukutana uso kwa uso na daladala hiyo iliyokuwa ikitokea Kibamba kuelekea Ubungo kabla ya kuburuzana hadi mtaroni na kulaliwa na lori hilo.

Sponsor ilishuhudia daladala hilo likiwa lime'banda' na kuwa mithili ya chapati huku miili ya watu iliyokuwa nayo imechanwa vibaya na mingine kutumbuka hadi utumbo kutoka nje ikiwa ndani yake.

Hili ni tukio la pili la aina yake katika kipindi cha miaka mitatu ukiachana na tukio jingine la aina hii lililowahi kutokea Kimara miaka mitatu iliyopta.

Hadi Sponsor inakwenda mitamboni bado zoezi la kuopoa miili hiyo lilikuwa linaendelea.

PICHA ZA TUKIO:


No comments:

Post a Comment