Friday, April 3, 2009

Kili Music Awards: Patakuwa hapatoshi!

Kesho ni kesho asemae leo ni muongo. lile shindano kubwa hapa nchini la tuzo za muziki za kilimanjaro lililokuwa linasubiriwa kwa hamu, limefikia patamu.

Leo nilitembelea katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambako ndiko kunatarajiwa kufanyika kwa shindano hilo, na nikajionea namna mafundi wakiwa katika hatua za mwisho mwisho za ujenzi wa jukwaa baab kubwa litakalotumika na wasanii wetu hapo kesho.

Bila shaka washabiki wa mambo ya burudani hasa za muziki watakuwa wamejipanga vilivyo kushuhudia shindano hilo. Labda kwa kuwakumbushia viingilio katika tuzo hizo ni shs 50,000/ kwa vip na shs 20,000/ kawaida.

No comments:

Post a Comment