Wednesday, April 29, 2009

MABOMU YATIKISA DAR

Milipuko ya mabomu yaliyokuwa yamehafadhiwa katika ghala la kutunzia silaha hizo ya Kambi ya Jeshi ya Mbagala Kizuiani imelitikisa jiji la Dar mapema aubuhi leo na kuendelea mpaka nyakati za mchana.

Mwana 'Sponsor' ambaye alikuwepo eneo la tukio alishuhudia wakazi wa maeneo hayo wakiyahama makazi yao kutokana na hofu kubwa iliyokuwa imetanda miongoni mwao. "Nilikuwa nimekaa chini hapa, ghafla nikasikia mlipuko mkubwa ambao sikuwahi kuusikia tangu nizaliwe." Alisema Mkazi mmoja wa eneo hilo.

Sponsor ilishuhudia vikosi mbalimbali vya ulinzi vya jeshi la Wananchi vikiwa katika eneo hilo kulinda usalama wa wananchi, na kuhakikisha wanadhibiti milipuko hiyo. "Haya mabomu ni kama mfano wa 'missile' (makombora), yanapolipuka husafiri umbali wa zaidi kilometa 10." Alisema mmoja wa askari wa JWTZ.

Katika Hospitali ya wilaya ya Temeke, hali ilikuwa ni ya majonzi baada ya hospitali hiyo kufurika majeruhi wa milipuko hiyowaliokuwa wamelala sakafuni na wengine wakionekana kupoteza fahamu kabisa.

Idadi kubwa ya majeruhi hao ni wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari, wengi wao wakiwa ni wasichana. Sponsor pia ilishuhudia wauguzi wa hospitali hiyo wakitoa huduma ya kwanza ambao walikuwa wakipigana vikumbo katika kordo za hospitali kwa kupokea miili ya majeruhi.

Ndugu na jamaa wa karibu wa majeruhi hao walionekana kutokwa na machozi, huku wengine kuchanganyikiwa wakiwa wanapepea majeruhi hao hospitalini hapo. Mpaka sponsor inakwenda mitambo, idadi ya majeruhi wa milipuko hiyo haikujulikana.


WAnajeshi wakilundika mabaki ya mabomu yaliyolipuka

No comments:

Post a Comment