Friday, April 10, 2009

Wakristo nchini watekeleza Ibada ya Ijumaa Kuu leo

Waumini wa dini ya Kikristo nchini na duniani kote leo wametekeleza Ibada ya Ijumaa kuu ya kumbukumbu ya kufa kwa Yesu Kristo msalabani kwa mujibu wa imani yao. Kwa hapa jijini ibada hiyo imefanyika katika makanisa mbalimbali yakiwemo Kanisa Kuu la Mt. Joseph, Kanisa la Azania Front pamoja na makanisa mbalimbali.

Ibada hiyo iliambatana na maigizo ya mateso ya Yesu Kristo, kwa mujibu wa imani ya waumini hao.



Vijana wa kanisa la Azania Front la jijini Dar es Salaam wakiigiza mateso ya Yesu Kristo, ikiwa ni moja ya Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika leo nchini kote na dunia nzima.

No comments:

Post a Comment