Friday, April 24, 2009

Walemavu wakiwezeshwa wanaweza..

BENKI ya Standard Chartered leo imetoa msaada wa kompyuta tatu kwa chama cha wasioona Tanzania (TLB), kupitia Shirika la Kimataifa la Wasioona (Sightsaver International) ikiwa ni moja ya malengo ya benki hiyo hapa nchini kusaidia jamii katika upande wa elimu.

Akizungumza na wahabarishaji katika makao makuu ya Shirika hilo, yaliyopo Mikocheni jijini hapa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha benki ya Standard Chartered, Lucy Kihwele amesema kuwa msaada huo wa kompyuta utakuwa ni changamoto kwa wahisani ndani na nje ya nchi kuwa walemavu ni wanajamii ka zilivyo jamii nyingine na pia wakiwezeshwa wataweza.

Alisema kuwa benki yake imedhamiria kuwasaidia walemavu nchini katika upande wa elimu na huo ukiwa ni mwanzo tu wa dhamira hiyo.


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kusaidia Wasioona (Sightsavers International), Dkt. Ibrahimu Kabole (kushoto) akionyesha namna kompyuta inavyoweza kutumiwa na mlemavu wa macho..

No comments:

Post a Comment