Wednesday, April 22, 2009

Ufukuaji mbegu DECI ni mbinde usipime...

Wanachama wa iliyokuwa kampuni ya upandaji na uvunaji mbegu (DECI Tanzania Ltd) leo walikusanyika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Mabibo, jijini kwa ajili ya kufukua mbegu zao ambazo nyingine bado hazijaanza kuota.

Sponsor ilifika eneo la tukio na kukuta maelfu ya wanachama hao wakiwa wameizunguka ofisi ya DECI huku wakisukumana kwa ajili ya kuingia ndani kufukua mbegu zao hizo. Hali haikuwa ya kuridhisha kwani msongamano huo ungeweza kuleta maafa kutokana na kila mmoja wao kutaka kuwa wa kwanza kungia kurudishiwa mbegu zake.

No comments:

Post a Comment