Thursday, May 14, 2009

MILIPUKO YA MABOMU- LIPUMBA ATAKA TUME HURU IUNDWE

KUFUATIA kutokea kwa milipuko ya mabomu wiki mbili zilizopita katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kambi ya Mbagala, Dar es Salaam, Chama cha Wananchi, CUF kupitia kwa Mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali iunde tume huru itakayochunguza chanzo cha milipuko hiyo.

Tume hiyo itashirikisha wataalamu wa mabomu toka nchi marafiki na Tanzania zikiwemo Ujerumani, Marekani na nyinginezo.

"Hatuielewi serikali kuhusiana na suala la ulipukaji wa mabomu Mbagala. Iundwe tume huru kutoka nje, ituambie ukweli." Alisema.

Aidha amewataka baadhi ya wafuasi wa vyama wanaotumia nafasi zao vibaya katika ugawaji wa vyakula vya misaada kwa waathirika hao kuacha aliouita ufisadi usio na huruma kwa waathirika wa milipuko hiyo, ambao wengi wao ni mama waja wazito, vikongwe na watoto wadogo.

Lipumba alifanya mkutano na waandishi wa habari leo asubuhi, katika ofisi za makao makuu ya chama chake cha CUF, kuzungumzia ajenda tatu ambazo ni Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Busanda, jimbo la Magogoni pamoja na Milipuko ya mabomu iliyotokea Mbagala wiki mbili zilizopita.


Prof. Lipumba akifafanua jambo leo. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad

No comments:

Post a Comment