Monday, May 4, 2009

Misaada zaidi yatolewa wahanga wa mabomu

MISAADA zaidi imeendelea kutolewa na wahisani mbalimbali kwa wahanga wa milipuko ya mabomu, ikiwasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Leo, Meneja Mkuu wa Kiwanda cha unga cha Bakhressa, Tawi la Mzizima, Said Abeid ametoa msaada wa shs Milioni 100 kwa niaba ya Makampuni ya Bakhresa, ambazo alikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi kwa ajili ya kusaidia wahanga wa milipuko ya mabomu, Mbagala.

Wakati huohuo, Jumuiya ya mabohora wa Tanzania wametoa hundi yenye thamani ya shs milioni 5.2 kwa Mkuu huyo wa mkoa kwa ajili ya kusaidia wahanga hao.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam William Lukuvi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini

No comments:

Post a Comment