Wednesday, May 13, 2009

UCHAGUZI MWINGINE JIMBO LA BIHARAMULO WAJA

WIKI chache baada ya kufariki kwa alyekuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi kwa tiketi ya TLP, Phares Kabuye kufariki dunia, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza rasmi kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa bunge katika jimbo hilo mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Rajabu Kiravu, uteuzi wa wagombea utaanza tarehe 9 mwezi Juni siku moja kabla ya Kampeni za Uchaguzi ambazo zitafanyika tarehe 10 mpaka 4 mwezi Julai, wakati shughuli za upiaji kura zitafanyika siku moja baa ya kumalizika kwa kampeni.


Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Rajab Kiravu

No comments:

Post a Comment