Sunday, May 10, 2009

Tunaadhimisha vipi Mothers day?

Habari za mchana wasomaji wa blog hii ya sponsor. Bila shaka wengi wenu mpo majumbani na wengine makazini na sehemu mbalimbali za kujipumzisha huku mkidodosa mawili matatu katika mitandao yenu.

Ndio, mambo yamebadilika siku, lazima twende na wakati, siku hizi kupata information ni rahisi kweli kuliko enzi zileee... nadhani mmenisoma. Kwa mtu ambaye atabisha basi huyo mbishi na mvivu totally!

Eh nsije kusahau, hivi leo ni Mothers day vile eenh? Au hata nyie hamjui? Ni kaweli leo ni mothers day. Lakini sasa tunaadhimisha vipi siku hii ya leo? Kwa kuwakumbuka mama zetu, na mama zetu kuwakumbuka sisi watoto zao basi au kuna jingine?

Kukumbukana kupo kwa njia mbalimbali.. kama kupeana zawadi mbalimbali ambazo ni maalumu. Maana wengine zawadi hizi wanashindwa kuzitoa kwa wakati maalumu.

Hebu mpatie mamayo au mwanao kitu ambacho akikitazama, atakuwa anakukumbuka siku zote hata kama utakuwa umeaga dunia. Hizi ni nafasi adimu sana kuzikuta katika maisha yetu. Kwa wale ambao mama zao wameshatangulia mbele ya haki, si mbaya sanana, wakawa wanawatilia ubani au kwa maana nyingine kuwafanyia dua ya kuwaombea heri na amani huko walipo, zote ni aina ya zawadi hizi.

Siku ya leo tuwafanyie mambo mazuri mama zetu, na pia nyiniy mama zetu leo mtupe raha ili kila mmoja wetu ajisikie kwamba kaadhimisha siku ya kina mama yaani 'Mothers day'.

No comments:

Post a Comment