Saturday, October 31, 2009

Simba 1 Yanga 0

Klabu ya Simba imeendeleza ubabe wake leo kwa timu za nyumbani baada ya kuichapa Yanga kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni...

Wadau walivyo'graduate' leo...


Wadau wa TSN (kutoka kushoto) Jamila Kilahama, Stella Nyemenohi na Maulid Ahmed wakitabasamu baada ya kutunukiwa shahada zao leo katika mahafali ya 21 ya chuo kikuu huria Tanzania, yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani..

Thursday, October 29, 2009

UMEME WA IPTL BADO KITENDAWILI

Umeme uliokuwa ukitarajiwa kuanza kuzalishwa na Kampuni ya kuzalisha nishati ya Umeme ya IPTL mwanzoni mwa mwezi ujao bado ni kitendawili kutokana na mitambo yake kutowashwa mpaka leo, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na blog hii.

Uchunguzi umebaini kuwa hata mafuta ya kuwashia mitambo hiyo bado hayajawasili eneo hilo.

Kwa mujibu wa mmoja wa 'staff' mmoja wa IPTL (jina kapuni), taratibu za kuanza kupakuwa mafuta yaliyoletwa na meli kwa ajili ya kuwashia mitambo hiyo, bado hazijafanywa.

"Unajua hapa mpaka wasafishe matenki yale, ndipo yawekwe mafuta kwa ajili ya kuwashia mitambo. Lakini mimi sijaona gari lolote la mafuta likileta hapa." Alisema.

Hivi karibuni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliwahakikishia wananchi kuwashwa kwa mitambo ya IPTL tarehe mosi ya mwezi Novemba itakayozalisha Megawati 100ahadi inayoonekana kutotekelezwa ipasavyo kutokana na mazingira ya kutatanisha yanayoonekana katika Kampuni hiyo.


mitambo ya IPTL ikionekana kutokuwa na dalili yoyote ya kuwashwa kama ilivyokutwa leo mchana

Miss Tourism Ilala at KIU University..


Washiriki wa Miss Tourism Ilala 2009 wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea chuo kikuu cha Kampala (Kampala International University- KIU), Dar es Salaam juzi

Wednesday, October 28, 2009

BOMU LAUA 90 PAKISTAN

Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari limelipuka na kuua watu 90, eneo la sokoni, Pashawar, nchini Pakistani leo idadi kubwa ikiwa ni wanawake, serikali imesema.

Mlipuko huo ambao umetokea katika Bazaar ya Meena umejeruhi zaidi ya watu 200, kwa mujibu wa Waziri wa Habari wa Jimbo la kaskazini Magharibi.

Inasemekana mlipuko huo utakuwa ni miongoni mwa milipuko mikubwa zaidi kutokea katika jimbo hilo likihusisha vifo zaidi vya kina mama.

FM Academia Kuipua Albamu mpya ya 'Vuta Nikuvute'

Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' wanatarajia kuzindua albamu yao mpya ya saba itakayokuwa ikiitwa 'Vuta Nikuvute' siku ya Ijumaa, katika ukumbi wa Heineken, Dar es Salaam.

Shein afungua Kongamano la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki


Makamu wa Rais, Ali Mohammed Shein (wapili kulia), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Bakari Mwapachu (kulia) na Maprofesa wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki linalojadili juu ya uwekaji mikakati ya maendeleo na usimamizi wa Elimu ya Juu katika ukanda wa Afrika

African Essence Magazine Launched last Night...


EAC, Secretary General, Amb. Juma Bakari Mwapachu displays a book titled 'African Essence' under the ALI East Africa Foundation, last night at Hotel Movenpick, Dar es Salaam. Second Right is a Chairman of the Foundation, Ali Mufuruki and the Secretary, Zuhura Muro (left side).

Tuesday, October 27, 2009

TASWIRA KATIKA JIJI...


Haya si mapambo bali ni matambara ambayo yananing'inia katika uzio wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam na kuleta taswira mbaya kwa wageni na wapitao kwa miguu.

Matambara haya ni mabango ambayo muda wake umeshakwisha lakini yameachwa hapa na hatimaye kuraruka na kupeperuka ovyo mithili ya bendera za nchi gani sijui... Haipendezi hata kidogo... Meseji sent!

Swissport wapigwa msasa

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport Tanzania Ltd, waliokuwa wamehudhuria mafunzo ya wiki moja ya Uhakiki wa Uzito waNdege na Mizania, leo wamekabidhiwa vyeti vyao baada ya kumaliza mafunzo hayo.


Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni za Swissport, Mozambique Airlines na Fast Track baada ya kukabidhiwa vyeti vyao leo

Tigo yakabidhi vifaa vya michezo

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ili kuiwezesha timu yake kufanya vema katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya shs milioni 6.8 ni pamoja na viatu vya mpira seti 2, jezi za netball 14, track suits jozi 44, jezi za mchezo wa riadha jozi 6, mipira ya miguu 10 na mipira ya pete 5.


Ofisa uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akikabidhi vifaa hivyo kwa Kamishna Uhamiaji anayeshughulikia Sheria, Wizara ya Uhamiaji na Mambo ya Ndani, Magnus Ulingi

Bunge laanza, Werema aapa


Spika wa Bunge, Samuel Sitta akiongozwa kufungua kikao cha 17 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano, mjini Dodoma jana.

Wednesday, October 21, 2009

RITA WAZINDUA CHETI KIPYA CHA KUZALIWA

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), leo imezindua cheti kipya cha kuzaliwa chenye alama za usalama. Cheti hicho ambacho ni vigumu kughushi kimezinduliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa Katiba na Sheria, MAthias Chikawe (kushoto)pamoja na Kaimu Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko wakibeba mfano wa cheti hicho kipya baada ya kuzinduliwa rasmi leo jijini.

JK AWAAPISHA ALIOWATEUA LEO IKULU


Rais Jakaya Kikwete (mbele katikati), Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein (kushoto) pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioapa jana. Kutoka kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Sazi Salula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, Katibu wa Rais, Prosper Mbena na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Christopher Sayi. Waliosimama nyuma ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peniel Lyimo.

Thursday, October 15, 2009

Wabunge wachafu kuanza kushughulikiwa

Kamati ya Halmashauri Kuu ya CCM inatarajia kuanza kazi ya kuwachunguza wabunge wenye mienendo isiyofaa katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu wa Kamati hiyo, Pius Msekwa amewaambia waandishi wa habari leo asubuhi wakati wa mkutano na wadau hao wa nyuzi, nyumbani kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Saturday, October 3, 2009

SIMBA HAIKAMATIKI, YANGA YAJISOGEZA...

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu ya soka ya Yanga leo imefuta uteja wa kurambishwa sukari na timu ya Kagera Sugar baada ya kuichapa kwa magoli 2-0katika mechi iliyochezwa uwanja wa Kaitaba, Bukoba leo, wakati Simba ya Dar es Salaam ambayo inaongoza Ligi ikishinda dhidi ya Moro United kwa magoli 2-1.


Mlinda mlango wa timu ya Moro United, Rajab Masud pamoja na Nahodha wake Wazir Mahadhi wakiangalia mpira ukiingia wavuni kuandika goli la kwanza, huku mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi akijiandaa kwa lolote litakaloweza kutokea wakati wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo

MISS TANZANIA: BADO KUNA TATIZO

Mrembo wa Tanzania 2009 Miriam Gerald amepatikana katika kinyang'anyiro kilichofanyika usiku wa kuamkia leo, jijini hapa Dar es Salaam. Tunaishukuru kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga 'Uncle' kwa kufanikisha hilo, na kuwa na moyo wa kujitolea tangu mbio hizo zilipoanza.

Pongezi hizo ziende sambamba na changamoto katika kamati hii ya Miss Tanzania, ambayo ni tatizo la kujieleza kwa washiriki wetu pindi inapofikia hatua ya maswali. Jana tulishuhudia baadhi ya warembo hao wakishindwa kujieleza vizuri mbele ya hadhira jambo lililopelekea wengine kutoa majibu yasiyoeleweka.

Nampongeza sana Miriam, ambaye ndiye Miss Tanzania 2009, kwa kujieleza vema kwa usahihi hasa alipoamua kutumia lugha ya kiswahili ambayo ndiyo ya Taifa, ambo lililompa uhuru wa kujieleza na kueleweka kwa majaji, na washabiki waliokuwa wamehudhuria mashindano hayo.

Mungu ibariki lugha yetu ya Kiswahuili, Mungu ibariki Tanzania!


Vodacom Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Beatrice Lukindo (kulia) na mshindi wa tatu Sia Ndasikoi, baada ya kutangzwa washindi wa shindano hilo Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo

Thursday, October 1, 2009

KWA WASOMAJI WA BLOGU HII

Ni muda mrefu sasa blogu yenu muipendayo ya Sponsor haikuwa 'updated' kutokana na sababu za kiufundi zinazoendelea kufanyiwa kazi na mtaalamu wa blogu hii.

Hivyo nachukua fursa hii kuwaomba radhi wasomaji wangu kutokana na usumbufu wowote unaoendelea kujitokeza, lengo ni kuboresha blogu hii ya Sponsor, ili wewe msomaji uweze kufaidika na habari motomoto.

Ahsanteni.

Akida. F. S
Managing Editor,
Sponsor.blogspot.com

KUMEKUCHA SERIKALI ZA MITAA


Wagombea wa nafasi za ujumbe wa serikali ya mtaa wa Kilakala, Yombo, Dar es Salaam wakipunga mikono walipowasili katika ofisi ya serikali ya mtaa kwa ajili ya kuchukua fomu, mapema leo asubuhi. Wa pili kulia ni shangazi yake mimi, Mariam Akida.

Shangazi yake mimi, Mariam Akida akikabidhiwa fomu ya ugombea nafasi ya ujumbe toka kwa ofisa mtendaji wa mtaa wa Kilakala.

BAYPORT YAGAWA JEZI MAMBO YA NDANI


Meneja Masoko wa Kampuni ya Bayport, Ngula Cheyo (kulia) akikabidhi jezi kwa Ofisa Utumishi anayeshughulikia Michezo, Wizara ya Mamabo ya Ndani ya Nchi, Felister Shuli, kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya klabu ya soka ya wizara hiyo, Dar es Salaam jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Michezo wa wizara, Staford Busumbiro.