Thursday, October 29, 2009

UMEME WA IPTL BADO KITENDAWILI

Umeme uliokuwa ukitarajiwa kuanza kuzalishwa na Kampuni ya kuzalisha nishati ya Umeme ya IPTL mwanzoni mwa mwezi ujao bado ni kitendawili kutokana na mitambo yake kutowashwa mpaka leo, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na blog hii.

Uchunguzi umebaini kuwa hata mafuta ya kuwashia mitambo hiyo bado hayajawasili eneo hilo.

Kwa mujibu wa mmoja wa 'staff' mmoja wa IPTL (jina kapuni), taratibu za kuanza kupakuwa mafuta yaliyoletwa na meli kwa ajili ya kuwashia mitambo hiyo, bado hazijafanywa.

"Unajua hapa mpaka wasafishe matenki yale, ndipo yawekwe mafuta kwa ajili ya kuwashia mitambo. Lakini mimi sijaona gari lolote la mafuta likileta hapa." Alisema.

Hivi karibuni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliwahakikishia wananchi kuwashwa kwa mitambo ya IPTL tarehe mosi ya mwezi Novemba itakayozalisha Megawati 100ahadi inayoonekana kutotekelezwa ipasavyo kutokana na mazingira ya kutatanisha yanayoonekana katika Kampuni hiyo.


mitambo ya IPTL ikionekana kutokuwa na dalili yoyote ya kuwashwa kama ilivyokutwa leo mchana

No comments:

Post a Comment