Tuesday, December 29, 2009

KIFIMBO KILIPOTUA IKULU KWA JK


MBIO ZA KIFIMBO CHA MALKIA KATIKA PICHA


Wavuvi nao katika Soko la Samaki Magogoni hawakuwa nyuma...

Utamaduni wa wahindi haukuachwa nyuma...

Rais wa TFF, Leodgar Tenga na Mkurugenzi wa TBC, Tido Muhando hawakuachwa nyuma...

Maafande wetu si tu wanapambana na wahalifu, lakini hata katika shughuli za kijamii wamo...

Tabasamu la Kifimbo cha Malkia...

Friday, December 25, 2009

KILAINI ATOA SOMO KUSHEREHEKEA KRISMASI

Aliyekuwa Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Methodius Kilaini amewaasa wazazi na walezi kusherehekea pamoja na familia zao Sikukuu ya Krismasi ambayo imeadhimishwa leo duniani kote na waumini wa dini ya Kikristo.

Kilaaini amesema ni vema kama unakwenda kusherehekea mbali na nyumbani ukabeba familia yako yote na si kuiacha nyingine ikiwa wapweke kwa kushindwa kusherehekea sikukuu hii.

Askofu Kilaini ametoa kauli hiyo wakati wa Ibada ya Misa ya Krismasi iliyofanyika kitaifa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam leo asubuhi.


Askofu Kilaini akizungumza na mtoto

Wednesday, December 9, 2009

TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 48 YA UHURU


Watoto wa Halaiki wakijipanga katika mistari iliyonyooka katika kuadhimisha Miaka 48 ya Uhuru wa Tanzania leo katika Uwanja wa Uhuru, jijini

Thursday, December 3, 2009

HAPA VIPI?


Kondakta wa dalada linalofanya safari zake kati ya Kimara na Kariakoo akipakia abiria sehemu ya kivuko cha watembea kwa miguu, Njia panda ya Mabibo, Urafiki. Hii si mara ya kwanza kwa makondakta na madereva wao kupakia na kushusha abiria sehemu hii jambo ambalo ni ukiukaji wa sheria za usalama barabarani.... Kamanda Kombe upo?

Thursday, November 26, 2009

URAFIKI WA MASHAKA...


Hawa jamaa walikutwa leo na Kamera yangu wakiwa katika mshikamano wa aina yake katika kituo cha Mabasi cha Ubungo jijini hapa... Hawa ni Masai na Mzungu...

TCC MLIPAKODI WA MWAKA

Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), leo mchana imekabidhiwa tuzo ya mlipakodi wa mwaka toka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, wakati wa maadhimisho ya nne ya mlipakodi nchini yaliyofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini hapa.

Mshindi wa kwanza wa ulipajikodi wa mwaka, mwakilishi wa TCC (kushoto) na Mshindi wa tatu mwakilishi wa benki ya CRDB wakiwa katika pozi

Mjomba 'mrisho mpoto' naye alikuwepo katika upande wa burudani...

Sunday, November 22, 2009

CHADEMA YAANZA KUPANGUKA TARATIIBU


Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi Taifa, James Mbatia akikabidhi kadi ya uanachama kwa mwanachama mpya ambaye awali alikuwa Ofisa Habari wa CHADEMA, DAvid KAfulila leo katika makao makuu ya chama hicho, Ilala Dar es Salaam

KARUME AANZA KAMPENI MAPEMA VISIWANI...


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume akipokea maandamano ya wananchi na wanachama wa Chama cha MapinduziCCM wa Mikoa Mitano ya Unguja, yaliyofanyika katika uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti Mkoa wa Mjini Magharibi jana.

SHOPPING INAENDELEA KAMA KAWAIDA MLIMANI CITY

Tamasha la 'Mlimani City Shopping Carnival' lililofunguliwa Ijumaa iliyopita katika viwanja vya Mlimani city, limeingia siku yake ya tatu leo.

Lengo la tamasha hilo ni kuwashawishi watanzania kujenga utamaduni wa kufanya shopping katika maduka makubwa na kuondoa dhana tofauti iliyojengeka miongoni mwao kwamba shopping katika maduka hayo 'Malls' 'Plazas' na hata Supermarkets hufanywa na watu weupe pekee...

Baadhi ya wajasiriamali wakiendelea kuuza bidhaa zao katika tamasha hilo leo mchana..

UBABE UNAPOHAMIA BARABARANI...

ELIMU YA AJABU NDANI YA MSITU

Unaweza ukastaajabu lakini ni kweli... Hili ni tukio la aina yake ambalo wengi wetu tumekuwa tukisikia tu kupitia vyombo mbalimbali vya habari na kadhalika... Katika hali isiyo ya kawaida Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya amewakuta watoto wadogo wakazi wa Kijiji cha Igumbiro, Tarafa ya Lupiro, Wilayani Ulanga zaidi ya kilometa 12 toka kijijini mwishoni mwa wiki wakifundishwa kusoma, kuandika, kuhesabu na kujua lugha ya kiswahili ndani ya Msitu wa hifadhi ya asili wa Nanji.

Watoto hao walikuwa wakifundishwa na mwalimu asiye rasmi aliyetambulika kwa jina la Msuya Shaaban.


Watoto hao wakiwa na mwalimu wao msituni...

Tuesday, November 17, 2009

WALIMU WA PRIMARY WENYE DIGRII ZAO KUPEWA SHAVU

Serikali imesema itatoa 'shavu' kwa walimu wa Primary wenye digrii zao kufundisha katika shule za Sekondari. Katibu Mkuu Kiongozi wa nchi, Philemon Luhanjo ameyasema hayo leo alipofanya mkutano na wadau wa mambo ya habari jijini hapa.


Katibu Mkuu kiongozi, Philemon Luhanjo akizungumza leo na waandishi wa habari

Monday, November 16, 2009

ANNE KILANGO AMWAGA MACHOZI SAME

Safari ilianza hivi:


Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela alianza safari yake ya kupanda mlima kuelekea kwenye maafa akisaidiwa na Mbunge wa Vunjo, Alloyce Kimaro (kulia).


Bada ya kushuhudia maafa hayo, Mbunge huyu alishindwa kujizuia na kuanza kuangua kilio hadharani... Lakini wamama wa kijijini pale walimfariji...


Hapa akina mama hawa wa kijijini hapo wakiendelea kumfariji Mama Anna kilango..


Baada ya hapo Mama Anne Kilango alimshukuru Mungu na kumuomba awalaze marehemu wote mahala pema peponi kama anavyoonekana...

Maporomoko ya Miamba yaliyotokea wiki iliyopita katika Kijiji cha Goha, Wilayani Same na kusababisha vifo vya watu 24 mpaka kufikia jana. Pia mali mbalimbali za wanakijiji hao ziliharibika ikiwamo mazao ya shambani, mifugo na kadhalika...

Mungu azilaze roho za Marehemu hao mahala pema peponi.

Saturday, November 14, 2009

Hivi ndivyo Mamba Myamba, Same ilivyoporomoka...







NB: Picha zote zinaonyesha harakati za ufukuaji miili ya marehemu waliofukiwa na miamba katika kijiji cha Goha, Mamba Myamba, Same mkoani Kilimanjaro kama zilivyopigwa na mdau wetu

Friday, November 13, 2009

MAHUJAJI WAKWAMA UWANJA WA NDEGE DAR

Zaidi ya Mahujaji 35 waliokuwa wasafiri kuelekea Makka kwa ajili ya Ibada ya Hijja wamekwama leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Sababu ya kukwama kwao ni kushindwa kufikia makubaliano yao na wakala wa ndege wa Kampuni ya Skylink ambao ndio waliokuwa wakishughulikia masuala yao ya safari.

HALMASHAURI ZA MIJI ZAKABIDHIWA MAGARI, PIKIPIKI NA PRINTERS

Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na wahisani wamekabidhi magari 57 aina ya Nissan Patrol, Pikipiki 407 pamoja na printers 286 kwa Halmashauri za miji Midogo, ofisi za Mabonde na ofisi za Wizara kwa ajili ya kusaidia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP), leo jijini hapa Dar es Salaam.


sehemu ya pikipiki 407 zilizotolewa na wizara

sehemu ya magari 57 yaliyokabidhiwa

Monday, November 2, 2009

SOMA HIYO KARATASI KWA MAKINI... OLE WAKO UKUTWE UKI... UTAWAJUA MGAMBO...

JK aipa changamoto Sekta ya Afya

Rais Jakaya Kikwete leo amefungua rasmi shule ya meno ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Tiba na Afya Muhimbili (MUHAS, jijini ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali yake ya kuboresha sekta ya Afya kwa nyanja zote.

Mbali na shule hiyo, pia Rais Kikwete alifungua huduma mbalimbali zitakazoanza kutolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zikiwemo matibabu ya figo na nyinginezo.

Rais Kikwete amesema Serikali yake imedhamiria kuboresha afya za wananchi kwa kuhakikisha inatoa fungu kubwa la fedha kugharamia zahanati za vijijini, kata na hospitali za wilaya.

"Afya za wananchi zikiwa bora, na maisha yao yatakuwa bora. Kila mtanzania apate huduma ya afya, tujenge vituo vya afya, zahanati karibu na wananchi." Alisema leo.

Rais Jakaya Kikwete, wadau wa afya na wataalamu mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na mashine ya kupima figo leo mchana Muhimbili

Saturday, October 31, 2009

Simba 1 Yanga 0

Klabu ya Simba imeendeleza ubabe wake leo kwa timu za nyumbani baada ya kuichapa Yanga kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni...

Wadau walivyo'graduate' leo...


Wadau wa TSN (kutoka kushoto) Jamila Kilahama, Stella Nyemenohi na Maulid Ahmed wakitabasamu baada ya kutunukiwa shahada zao leo katika mahafali ya 21 ya chuo kikuu huria Tanzania, yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani..

Thursday, October 29, 2009

UMEME WA IPTL BADO KITENDAWILI

Umeme uliokuwa ukitarajiwa kuanza kuzalishwa na Kampuni ya kuzalisha nishati ya Umeme ya IPTL mwanzoni mwa mwezi ujao bado ni kitendawili kutokana na mitambo yake kutowashwa mpaka leo, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na blog hii.

Uchunguzi umebaini kuwa hata mafuta ya kuwashia mitambo hiyo bado hayajawasili eneo hilo.

Kwa mujibu wa mmoja wa 'staff' mmoja wa IPTL (jina kapuni), taratibu za kuanza kupakuwa mafuta yaliyoletwa na meli kwa ajili ya kuwashia mitambo hiyo, bado hazijafanywa.

"Unajua hapa mpaka wasafishe matenki yale, ndipo yawekwe mafuta kwa ajili ya kuwashia mitambo. Lakini mimi sijaona gari lolote la mafuta likileta hapa." Alisema.

Hivi karibuni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliwahakikishia wananchi kuwashwa kwa mitambo ya IPTL tarehe mosi ya mwezi Novemba itakayozalisha Megawati 100ahadi inayoonekana kutotekelezwa ipasavyo kutokana na mazingira ya kutatanisha yanayoonekana katika Kampuni hiyo.


mitambo ya IPTL ikionekana kutokuwa na dalili yoyote ya kuwashwa kama ilivyokutwa leo mchana

Miss Tourism Ilala at KIU University..


Washiriki wa Miss Tourism Ilala 2009 wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea chuo kikuu cha Kampala (Kampala International University- KIU), Dar es Salaam juzi

Wednesday, October 28, 2009

BOMU LAUA 90 PAKISTAN

Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari limelipuka na kuua watu 90, eneo la sokoni, Pashawar, nchini Pakistani leo idadi kubwa ikiwa ni wanawake, serikali imesema.

Mlipuko huo ambao umetokea katika Bazaar ya Meena umejeruhi zaidi ya watu 200, kwa mujibu wa Waziri wa Habari wa Jimbo la kaskazini Magharibi.

Inasemekana mlipuko huo utakuwa ni miongoni mwa milipuko mikubwa zaidi kutokea katika jimbo hilo likihusisha vifo zaidi vya kina mama.

FM Academia Kuipua Albamu mpya ya 'Vuta Nikuvute'

Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' wanatarajia kuzindua albamu yao mpya ya saba itakayokuwa ikiitwa 'Vuta Nikuvute' siku ya Ijumaa, katika ukumbi wa Heineken, Dar es Salaam.

Shein afungua Kongamano la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki


Makamu wa Rais, Ali Mohammed Shein (wapili kulia), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Bakari Mwapachu (kulia) na Maprofesa wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki linalojadili juu ya uwekaji mikakati ya maendeleo na usimamizi wa Elimu ya Juu katika ukanda wa Afrika

African Essence Magazine Launched last Night...


EAC, Secretary General, Amb. Juma Bakari Mwapachu displays a book titled 'African Essence' under the ALI East Africa Foundation, last night at Hotel Movenpick, Dar es Salaam. Second Right is a Chairman of the Foundation, Ali Mufuruki and the Secretary, Zuhura Muro (left side).

Tuesday, October 27, 2009

TASWIRA KATIKA JIJI...


Haya si mapambo bali ni matambara ambayo yananing'inia katika uzio wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam na kuleta taswira mbaya kwa wageni na wapitao kwa miguu.

Matambara haya ni mabango ambayo muda wake umeshakwisha lakini yameachwa hapa na hatimaye kuraruka na kupeperuka ovyo mithili ya bendera za nchi gani sijui... Haipendezi hata kidogo... Meseji sent!

Swissport wapigwa msasa

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport Tanzania Ltd, waliokuwa wamehudhuria mafunzo ya wiki moja ya Uhakiki wa Uzito waNdege na Mizania, leo wamekabidhiwa vyeti vyao baada ya kumaliza mafunzo hayo.


Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni za Swissport, Mozambique Airlines na Fast Track baada ya kukabidhiwa vyeti vyao leo

Tigo yakabidhi vifaa vya michezo

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ili kuiwezesha timu yake kufanya vema katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya shs milioni 6.8 ni pamoja na viatu vya mpira seti 2, jezi za netball 14, track suits jozi 44, jezi za mchezo wa riadha jozi 6, mipira ya miguu 10 na mipira ya pete 5.


Ofisa uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akikabidhi vifaa hivyo kwa Kamishna Uhamiaji anayeshughulikia Sheria, Wizara ya Uhamiaji na Mambo ya Ndani, Magnus Ulingi

Bunge laanza, Werema aapa


Spika wa Bunge, Samuel Sitta akiongozwa kufungua kikao cha 17 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano, mjini Dodoma jana.

Wednesday, October 21, 2009

RITA WAZINDUA CHETI KIPYA CHA KUZALIWA

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), leo imezindua cheti kipya cha kuzaliwa chenye alama za usalama. Cheti hicho ambacho ni vigumu kughushi kimezinduliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa Katiba na Sheria, MAthias Chikawe (kushoto)pamoja na Kaimu Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko wakibeba mfano wa cheti hicho kipya baada ya kuzinduliwa rasmi leo jijini.

JK AWAAPISHA ALIOWATEUA LEO IKULU


Rais Jakaya Kikwete (mbele katikati), Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein (kushoto) pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioapa jana. Kutoka kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Sazi Salula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, Katibu wa Rais, Prosper Mbena na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Christopher Sayi. Waliosimama nyuma ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peniel Lyimo.

Thursday, October 15, 2009

Wabunge wachafu kuanza kushughulikiwa

Kamati ya Halmashauri Kuu ya CCM inatarajia kuanza kazi ya kuwachunguza wabunge wenye mienendo isiyofaa katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu wa Kamati hiyo, Pius Msekwa amewaambia waandishi wa habari leo asubuhi wakati wa mkutano na wadau hao wa nyuzi, nyumbani kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.