Uchunguzi uliofanywa na blogu hii katika Soko la Samaki Magogoni, jijini Dar es Salaam umebaini kuwa kila mfanyabiasharaanajipangia bei yake ya samaki pasipo kuwa na udhibiti wa bei hizo kutoka kwa Menejimenti ya Soko.
Jumanne Muchande ambaye ni muuzaji wa samaki aina ya Tasi na Changu anasema kuwa kwa sasa bei ya samaki sokoni hapo ipo chini kutokana na kupatikana kwa wingi, wakati Baltazar Ramadhan ambaye pia ni muuzaji wa samaki sokoni hapo anasema kuwa bei ipo juu na upatikanaji wake ni haba ukilinganisha na awali.
Baltazar akiwaandaa samaki wake katika eneo lake.
Kutokana na mkanganyiko huo, kila mfanyabiashara sasa anauza kwa bei yake kulingana na manunuzi ambapo Jumanne Muchande yeye anauza kwa bei ya chini wakati Baltazar anauza kwa bei ya juu kwa madai ya uhaba wa upatikanaji wake.
Kwa hali hii kuna haja ya wanunuzi kuwa ‘selektiv’ wachaguzi na kuacha papara pindi waendapo sokoni hapo ili kuepuka kuuziwa kwa bei kubwa ambapo unaweza kupata kwa bei ndogo kwa ukubwa, ubora na viwango sawa.
Wafanyabiashara wa samaki wakiandaa majokofu kwa ajili ya kuhifadhia samaki wao.
Samaki aina ya Changu, Tasi na jamii ya Jodari na Tasi wakisubiri wanunuzi.
No comments:
Post a Comment