Thursday, January 14, 2010

Waliokufa kwa Mafuriko Haiti wafikia 50,000

Zaidi ya watu 50,000 wanahofiwa kufa katika tetemeko kubwa kuliko yote yaliyowahi kutokea katika Kisiwa cha Haiti, wakati timu ya uokoaji toka Uingereza ikiwa imeungana na waokoaji wengine.

Mamilioni ya watu wanahitaji msaada wa haraka ambao tayari umeanza kutolewa na nchi mbalimbali.

Rais Barack Obama wa Marekani aliahidi kuziomba nchi mbalimbali duniani kutoa misaada yote ya kibinadamu kusaidia wananchi wa Haiti kuondokana na Maafa hayo yaliyotokea.

Wakati huohuo zaidi ya wataalamu 70 wa uokoaji pamoja na Mbwa pamoja na zana hevi zimewasili katika Uwanja wa Ndege wa Gatwick usiku wa jana, zilizotolewa na Serikali ya Ulaya.


Eneo lililokumbwa na mfurio linavyoonekana kwa juu

waathirika wa mafuriko wakiwa katika eneo moja la hifadhi

No comments:

Post a Comment