Tuesday, January 26, 2010

INDIA WASHEREHEKEA MIAKA 61 YA MUUNGANO

Raia wa Tanzania wenye asili ya India leo wamesherehekea Miaka 61 ya Muungano wa nchi yao katika Ofisi ya Ubalozi wa nchi hiyo iliyopo jijini hapa Dar es Salaam.



Balozi wa nchi hiyo Tanzania, Kocheril Bhagirath akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa nchi yake imeazimia kujenga miradi mikubwa hapa nchini ya Kielimu na Afya kwa lengo la kunufaisha watanzania.

Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Kituo Kikubwa cha Afya cha Kimataifa kitakachogharimu zaidi ya dola Milioni 20 za Marekani pamoja na Mradi mwingine wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambapo watanzania watapatiwa elimu ya Kompyut pamoja na Ajira.

No comments:

Post a Comment