Thursday, January 21, 2010

KAWAMBWA, NAGU NA MKULO WAIBUKA BANDARINI

Dar es Salaam,
Mawaziri watatu wenye dhamana nyeti katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Shukuru Kawambwa wa Miundombinu, Dk. Mary Nagu wa Viwanda na Biashara na Mustafa Mkulo wa Fedha na Uchumi wamefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam inayomilikiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kujionea utekelezaji wa shughuli zake leo jiji hapa.

Mawaziri hao walitembelea katika eneo lililokuwa likimilikiwa na NASACO ambalo kwa sasa lipo chini ya TPA na Kituo cha Kusafirishia Mafuta kujionea shughuli zinavyofanyika na mwisho kurejea katika chumba cha Mikutano kwa ajili ya kutoa Muhtasari kwa waandishi wa Habari.


Mawaziri, k. Shukuru Kawambwa wa Miundombinu na Dk. Mary Nagu wa Viwanda na Biashara wakiwa katika ziara hiyo leo

No comments:

Post a Comment