Monday, January 18, 2010

JK ASHTUKIA DILI, ACHOMOA KUKABIDHI GARI

Katika hali isiyotarajiwa na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliojitokeza kushuhudia tukio la makabidhiano ya magari mawili ya Wagonjwa 'Ambulance' Ikulu, Dar es Salaam, Rais Jakaya Kikwete alikataa kukabidhi moja ya magari hayo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Kayange Jacob baada ya kubaini kuwa si mlengwa wa gari hilo.

Mambo yalikuwa hivi;
Mapema mnamo saa sita na nusu za mchana, wandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliwasili Ikulu. Baada ya muda, Rais Kikwete naye aliwasili kwa ajili ya kukabidhi gari kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido (aliyemtarajia).

Waandishi wa habari walikuwa wamejipanga na kujiandaa na kamera zao tayari kwa kuchukua tukio hilo. Mkurugenzi yule naye ambaye hakuwa kusudio la Rais Kikwete naye alikuwa kajiandaa kwa kukabidhiwa gari lake.

Rais Kikwete alipokaribia eneo la tukio, akaanza kusalimia watu na kisha kuuliza, "We bwana unatokea wapi?, alimuuliza. "Natokea Ngorongoro mzee, " Alijibu. Rais Kikwete kama utani vile akazungumza, "Gari siyo yako bwana... Hii ni Kashfa kubwa, sikukabidhi gari bwana, gari hii wanatakiwa kukabidhiwa wanakijiji wa Engarinaibo na wala si Loliondo."

Baada ya hapo Rais Kikwete aliendelea kuhoji juu ya suala hilo, kisaha huyoooo akarudi zake ndani ya Ikulu na kuachwa maswali kibao kwa wandishi wa habari waliokuwepo pale pamoja na Mkurugenzi huyo naye asijue afanye nini baada ya kavukavu na Rais Kikwete.

Kwa hakika tukio hilo lilizua mijadala mikali kwa wandishi wa habari waliokuwepo eneo hilo mpaka wanaondoka.... Hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa ndugu msomaji.

Kwa uhondo zaidi tazama mfululizo wa tuki lenyewe katika picha hapo chini;


Magari yaliwasili katika viwanja vya Ikulu...


Punde Jk naye aliwasili tayari kwa kukabidhi


Baada ya hapo akamsalimia Mkurugenzi huyo na kuanza kumuhoji...


Baada ya kumuuliza mawili matatu akashangaa kulikoni...


Akazidi kusisitiza kuwa hakabidhiwi mtu gari hapa kama hahusiki...


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ngorongoro kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka asijue la kufanya baada ya kupewa kavukavu za usoni na JK...

No comments:

Post a Comment