Thursday, January 14, 2010

HAKUNA WA KUNINYIMA USINGIZI JIMBONI- WASSIRA

Waziri wa Kilimo na Chakula, Steven Wassira amesema hata kama kuna wagombea ambao wamejitokeza kushindana nae katika Jimbo lake, hawamnyimi usingizi na kutamba kuwa atalitetea jimbo lake kutokana na kukubalika na wananchi.

"Unajua mwenye dhamana ya Jimbo ni mwananchi, hivyo yeye ndiye anayejua yupi wa kumpa kura yake kulingana na kipi alichokifanya jimboni humo,

"Hao waliojitokeza kushindana na mimi nawajua vizuri sana. Ndio walewale wa mwaka 2005 niliokuwa nashindana nao, hivyo hawaninyimi usingizi hata kidogo."

Wassira alikuwa akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake Dar es Salaam jana kuhusu hali ya Kilimo na Chakula iliyopo sasa kutokana na mvua zilzioanza kunyesha.

No comments:

Post a Comment