Sunday, January 17, 2010

THE DREAM COME TRUE... SIMBA YAENDELEZA USHINDI



THE DREAM COME TRUE... Ndivyo usemavyo Ujumbe wa bango hili huku mshabiki wa klabu ya Simba akiwa na bendera yake juu ya bango hilo kusubiria kutimia kwa ndoto hiyo...

Ndoto ilitimia kweli baada ya Klabu hiyo kuichapa Majimaji kwa magoli 2-0 na hivyo kuendeleza rekodi yake ya ushindi wa kutokufungwa wala kutoa sare na timu yoyote inayoshiriki michuano hiyo.

Mechi hiyo ilifanyika jana katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salam ambapo Mshambuliaji hatari wa Simba, Mussa Hassan Mgosi aliipatia klabu yake hiyo magoli yote mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili.

No comments:

Post a Comment