Sunday, January 24, 2010

NDEGE KUBWA YA ABIRIA YATUMBUKIA BAHARINI

Ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Ethiopia, Boeing 737- 800 iliyokuwa imebeba abiria 92 na wafanyakazi imetumbukia baharini muda mfupi baada ya kuruka kutoka Beiruti kufuatia hali mbaya ya hewa.



"Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia yenye namba 409 imepata ajali muda mfupi baada ya kuruka majira ya saa 8.30 usiku ikiwa na abiria 83 wakiwemo wafanyakazi 9 wa ndege hiyo," Kwa mujibu wa taarifa ya ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Lebanon.

"Mashuhuda waliona mpira wa moto wakati ndege hiyo inatumbukia baharini," Aliendelea.

Ofisa huyo amesema kuwa waokoaji walijaribu kufika katika ndege hiyo kuona endapo watafanikiwa kukuta waliosalimika.

No comments:

Post a Comment