Tuesday, March 31, 2009

Mazishi ya Marehemu Hamidu Bisanga katika Picha


Waumini wakiswalia jeneza lenye mwili wa marehemu Bisanga kabla ya maziko


Jeneza lenye mwili wa marehemu Bisanga likiwa garini kuelekea makaburini


ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Bisanga kwa ajili ya maziko katika makaburi ya Kisutu..


Safari ya marehemu Hamidu Bisanga ilihitimishwa kwa kuuzika mwili wake katika kaburi hili..
Mungu ailaze roho ya marehemu Hamidu Bisanga mahala pema peponi, Amina!

Mamia wamzika Bisanga

Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam pamoja na maeneo mengine ya jirani, leo wamejitokeza kwa wingi kumsindikiza aliyekuwa mwandishi wa habari wa siku nyingi ndani na nje ya nchi, marehemu Hamidu Bisanga katika nyumba yake ya milele, makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.

Marehemu Bisanga alifariki dunia hivi karibuni kwa ajali ya gari, maeneo ya Makumbusho, Dar es Salaam.


Ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu Bisanga wakiwa wamebeba jeneza...

Friday, March 27, 2009

Wezi wa miundombinu ya maji sasa kukiona- DAWASA, DAWASCO

Sasa unaweza kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0756 889 930 pamoja na 0756 444 266, kuitaarifu DAWASCo nani ni mwizi wa miundombinu ya maji. Hii imetokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi wa miundombinu ya maji hapa jijini jambo linalopelekea wananchi wengine kukosa huduma hii muhimu.


Mkurugenzi wa ufundi wa DAWASA, Boniphace Kasiga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo, kuhusu kampeni kabambe ya wizi wa miundombinu ya maji...

Tuesday, March 24, 2009

SUMATRA YAIPIGA STOP SEAGULL KUSAFIRISHA ABIRIA

Mamlaka ya dhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA), imeipiga stop meli ya Seagull kubeba abiria mpaka hapo itakapokuwa imefanyiwa matengenezo.

Kwa mujibu wa barua yake iliyoiandikia kampuni hiyo, SUMATRA imesema seagull itaendelea na safari zake tu endapo itaridhishwa na maendeleo ya meli hiyo kupitia kwa mkaguzi alieidhinishwa.


Baadhi ya wafanyakazi wa Seagull wakiengalia sehemu ya meli ya seagull iliyoharibika


Meli ya Seagull ikiwa imetia nanga baada ya kuzuiwa kusafiri


Abiria wa Seagull wakirusha chupa za maji baada ya meli hiyo kupigwa stop kusafiri

OBAMA KUZUNGUMZIA UCHUMI WA MAREKANI LEO

Rais Barack Obama wa Marekani leo anatarajia kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mikakati ya maendeleo ya uchumi kwa nchi yake tangu aliposhika madaraka.

PINDA AZINDUA KONGAMANO LA USOMAJI VITABU AFRIKA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo amezindua kongamano la usomaji vitabu kwa nchi za Afrika, leo hapa jijini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi amesema kuwa waafrika hususan watanzania hawana budi kusoma vitabu ili kuondokoana na ujinga, umasikini na maradhi.

"Ujinga, umasikini na maradhi pia huchangiwa na kutosoma vitabu." Alisema.

baadhi ya washiriki wa mkutano wa usomaji vitabu kwa nchi za Afrika

Monday, March 23, 2009

Athumani azidi kupata nafuu


Mpigapicha wa magazeti ya Serikali (Dailynews na Habari leo), Athumani Hamisi akionekana mwenye tabasamu pamoja na wafanyakazi wenzake waliokwenda kumjulia hali nchini Afrika ya Kusini.

BAA TANO ZATINGA FAINALI NYAMA CHOMA

Baa tano hapa jijini zimefanikiwa kutinga katika fainali ya shindano la Nyama choma na Safari Lager.

Akizitaja baa hizo, Meneja Mkuu wa bia ya safari, Fimbo Butala amesema kuwa ni pamoja Titanic iliyopo Vingunguti, Kisuma ya Temeke, Nguruko ya Mbezi beach, Africentre ya Ilala pamoja na Madrid Pub ya Tegeta.

Mwishoni mwa wiki hii kunatarajiwa kufanyika kwa fainali hizo katika Viwanja vya Leaders.


Meneja wa bia ya Safari, Fimbo Butala (kushoto) akifafanua jambo

MOTO WAWAKA DAR, PWANI

Hoteli ya Paradise imeteketea kwa moto leo asubuhi huko Bagamoyo mkoa wa Pwani. Ni hali ya majonzi iliyotawala katika eneo hilo la hoteli ambapo baadhi ya wapangaji wake walionekana kubeba mizigo yao vichwani na kutimkia huku na kule.

Halikadhalika jijini hapa, moto umeteketeteza nyumba moja katika eneo la mtoni kijichi.


baadhi ya zilizzokuwa nyumba za makuti za hoteli ya Paradise zikionekana baada ya kuteketea kwa moto

Friday, March 20, 2009

LIPUMBA AKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUJADILI KUYUMBA KWA UCHUMI WA DUNIA


Mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akisisitiza jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani) wakati wa mjadala kuhusu kuyumba kwa uchumi wa dunia, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri nchini, Sakina Datoo.

TUZO ZA MWANDISHI BORA WA MWAKA ZAZINDULIWA

Baraza la Habari Tanzania (MCT), kwa kushirikiana na vyama sita vya waandishi wa habari pamoja na Kampuni ya Shaba and Associates leo vimesaini mikataba ya makubaliano kuhusu kuanzishwa kwa tuzo za mwandishi bora wa mwaka.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mara baada ya utiaji saini, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga amesema hii italeta changamoto kwa wana taaluma wa habari kufanya kazi yao kwa juhudi kubwa ukilinganisha na sasa.


MCT-Executive secretary, Kajubi Mukajanga (left) signs a MoU of the Journalist of the Year Awards with Shaba &Associates CEO, Richard Shaba today

Thursday, March 19, 2009

YANGA YAIFUNGA POLISI MORO KWA TAABU...


Mchezaji wa timu ya Polisi ya Morogoro, Adamu Juma akianguka nyuma ya Athumani Idi wa Yanga na kuunawa mpira jambo lililopelekea mwamuzi kutoa peneti iliyozaa bao pekee kwa timu ya Yanga, wakati wa mechi ya ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo alasiri.

KARIBU NYUMBANI JK...


Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mikono wananchi (hawapo pichani) waliojitokeza kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, akitokea ziarani nchini Uingereza. Kulia kwake ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

DUH! MGAMBO KUTOKA WAMACHINGA MPAKA BAA...

Katika hali ya kushangaza Kamera yangu ya 'Sponsor' iliwanasa mgambo wa jiji wakiwa wamevamia katika baa moja ya 'Honey Pub' eneo la Sinza Makaburini, na kulumbana na wahudumu kutokana na kilichoelezwa kuwa walikuta wateja wakinywa pombe muda ambao Serikali imepiga marufuku.

Baada ya malumbano yaliyochukua takribani saa nzima, ghafla nilishuhudia mgambo wale wakisomba baadhi ya viti vya wateja, kwa madai kuwa muhusika wa 'kaunta' waliyekuwa wakimuhitaji hakuwepo.

Chini ni picha mbalimbali za mgambo hao wakiwa katika eneo la tukio....


hapa walikuwa wakihesabu viti ili waondoke navyo


wakati wengine wakiendelea na zoesi la kuhesabu, huku wengine walikuwa na kazi na wamachinga wa cd waliokutwa katika baa hiyo...


baada ya kuvihesabu wanaondoka navyo sasa...

TLP KUMEKUCHA....

Chama cha siasa cha Tanzania Labour (TLP), leo kimetoa fursa kwa wananchama wake wawili kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Uenyekiti ambayo kwa sasa bado inashikiliwa na Agustino Lyatonga Mrema.

Joram Kinanda ambaye ni Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa TLP anasema "Ni muda muafaka sasa mheshimiwa Mrema kung'atuka atuachie na sisi nafasi za kukiongoza Chama."

Naye Katibu Mwenezi wa chama hicho, Benedicto Mutungirehi amelalamikia kitendo cha kutenguliwa ujumbe wa kukiwakilisha chama hicho katika vikao vya Kituo cha Sheria nchini -TCD, na kusema kuwa hizo ni njama dhidi yake za kumkatisha tamaa katika uchaguzi.


Katibu Mkuu Taifa wa TLP John Komba (kulia) akikabidhi fomu kwa Joram Kinanda

Wednesday, March 18, 2009

WASHIRIKI 2009 KILI MUSIC AWARDS WATAJWA...

Akitaja majina hayo pamoja na makundi, Mwenyekiti wa shindano hilo John Dilinga 'DJ JD' amesema wananchi wanatakiwa kuwapigia kura washiriki kwa kutuma namba zao za ushiriki kwa njia ya ujumbe mfupi pamoja na barua pepe kwenda vote@kilitimetz.com.

Miongoni mwa majina yaliyopendekezwa ni pamoja na nguli wa muziki Lady Jay dee, Matonya, Jahazi Modern Taarab, African Stars, Fm Academia, na wengineo wengi.

Katika tuzo hizo jumla ya makundi 20 yameteuliwa yakiwemo Mwimbaji Bora wa Kike, Mwimbaji Bora wa Kiume, Albamu bora ya Taarab, Wimbo bora wa Taarab, Wimbo wa Mwaka, Wimbo Bora wa Kiswahili na mengineyo.


Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Oscar Shelukindo (katikati) akionyesha kipeperushi kwa waandishi wa habari leo mchana baada ya uzinduzi...

'MSINIPIMIE KABISA' -Mwakyembe

Mbunge wa jimbo la Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe amevijia juu vyombo vya habari vilivyomwandika kuhusu suala la umilikaji wa baadhi ya makampuni.

"Tena niwaambieni kitu, hiki mlikuwa hamkifahamu kabisa... Mimi nina makampuni, na sio kampuni. Mimi msinifananishe na baadhi ya viongozi wanaotembeza bakuli...' Alisema.


Dk. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo asubuhi

Tuesday, March 17, 2009

TWANGA WATOA MSAADA HOSPITALI MWANANYAMALA..

Uongozi wa Makampuni ya ASET, inayomiliki bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta leo ulifanya ziara katika hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia wagonjwa na watoto waliolazwa hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka amesema ni vema wananchi wakajenga utamaduni wa kutembelea hospitali na kutoa misaada kwa wagonjwa wakiwa ni sehemu ya jamii.

Aidha amezitaka kampuni na wafadhili mbalimbali kuiga mfano wao, kwa kujijengea utamaduni wa kuwasaidia wagonjwa katika hospitali mbalimbali ili kuwapa faraja na ahueni ya kupona haraka ili warejee kuwa pamoja na familia zao pamoja na kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

"Ni wajibu wetu wanajamii kujitokeza na kutoa misaada kwa wagonjwa." Alisema.


Katibu wa bendi ya Twanga Pepeta, Abuu Semhando (wa pili kushoto) akikabidhi moja ya msaada kwa Muuguzi mwandamizi wa hospitali ya Mwananyamala, Angelina Saguti

Monday, March 16, 2009

HOFU YATAWALA MUSWADA MPYA WA SHERIA YA WANYAMAPORI AFRIKA MASHARIKI..

Muswada wa sheria ya wanyamapori na utalii wa bunge la Afrika Mashariki unatarajiwa kupelekwa Bungeni, baada ya wadau mbalimbali wa sekta hiyo kutoa maoni yao na michango mbalimbali juu ya muswada huo, jijini Dar es leo mchana...

Miongoni mwa maoni yaliyotolewa na wadau ni pamoja na suala la ushindani wa kibiashara, tatizo la lugha ya mawasiliano, na mengine mengi ambapo wamesema muswada huo utakapopitishwa utaleta changamoto kwa nchi ambazo hazijajitangaza zaidi katika Utalii.

Miongoni mwa nchi hizo walizozitaja ni pamoja na Tanzania, Rwanda na Burundi.


Mwenyekiti wa kamati ya Kilimo na Utalii ya Bunge la Afrika Mashariki, Dk. George Nangale akionyesha muswada wa sheria mpya kwa wadau leo jijini..

JK USO KWA USO NA BALOZI MAAJAR WA TANZANIA UINGEREZA


Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Maajar akikaribisha Rais Jakaya Kikwete baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Heathrow kuhudhuria kikao cha Pre-G20 mjini London.

Nyamachoma ya Safari yawashika wengi..

Shindano la Nyamachoma na Safari Lager, la Kampuni ya bia Tanzania-TBL, limevuta hisia za wengi baada ya baa nyingi zinazoshiriki kupata wateja wengi wa nyama ukilinganisha na kipindi cha nyuma.



Baadhi ya majaji wakionja nyama katika moja ya baa zinazoshiriki shindano la Nyamachoma





Thursday, March 12, 2009

WIZI WA SAMAKI- MAHAKAMA YAHAMIA BANDARINI

Hatimaye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imelazimika kwenda kuwasomea mashtaka yao watuhumiwa wa wizi wa samaki katika bahari ya hindi, eneo la Tanzania bandarini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa mahakama hiyo.

Sababu hizo ni pamoja na kushindwa kufika kwa wahandisi wa meli ya uvuvi ya Al Tawariq 1 mahakamani hapo kusomewa mashtaka yao, kutokana na kushindikana kuzima injini za meli hiyo, na hivyo mahakama kulazimika kwenda bandarini.


Watuhumiwa wa wizi wa samaki katika bahari ya Hindi wakiwa mahakamani leo


Watuhumiwa wa wizi wa samaki wakiwa chini ya ulinzi mkali kuelekea bandarini...

HUKUMU YA ALIEMZABA RAIS MWINYI KOFI KESHO..

Mtuhumiwa katika kesi ya kumshambulia Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Ibrahimu Said 'ustaadh' anatarajia kufikishwa tena Mahakamani kesho kwa ajili ya kusomewa hukumu yake baada ya leo kushindikana.

Awali Ibrahimu ambaye alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo asubuhi alikiri kosa lake mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, jambo lililorahisisha kuifanya kesi imalizike haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kupandishwa kizimbani, Ibrahimu ameiomba mahakama imuachie huru ili akasome na kuongeza kuwa haikuwa dhamira yake kumzabua kofi Rais Mwinyi.

"Naomba mahakama iniachie huru nikasome. Namuomba mzee (Mwinyi) anifutie hii kesi." Alisema.

Wakati huohuo, mama mzazi wa mtuhumiwa huyo, Mama Rehema Ngoma ambaye alionekana kuchanganyikiwa muda mfupi baada ya mwanaye kurudishwa rumande alisema Ibrahimu alipata msukosuko wa ubongo akiwa mdogo jambo linalomfanya wakati mwingine kuchanganyikiwa.


Ibrahimu Said 'Ustaadh' (kulia) akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu leo

Mama Mzazi wa Ibrahimu Said 'Ustaadh', Mama Rehema Ngoma akizungumza kwa jazba na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mwanaye kurudishwa rumande...

Wednesday, March 11, 2009

Tukio la Mwinyi kuzabwa kofi katika picha...

Ilianza kama muvi baada ya dogo kumzaba kibao Rais Mwinyi...

Wananchi wenye hasira nusura wamtoe roho kwa kipigo takatifu...

Bahati yake nzuri wanausalama walimwokoa toka kipondoni...

Akatolewa nje... wananchi wakamtolea mimacho...

Kinyozi alamba dume TIGO...

Mkazi wa Vingunguti, Dar es Salaam ambaye ni fundi kinyozi, Christopher Damian ameibuka kidedea kwa kunyakua shilingi milioni 3.8/- za promosheni ya mapenzi ya kampuni ya simu za mkononi, Tigo, Dar es Salaam leo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Christopher amesem "Sifikirii kufanyia chochote kwa sasa. Kwani sikutegemea kama nitashinda." Alisema.

Washindi wengine wanne waliojinyakulia zawadi mbalimbali ni pamoja na Elpidius Katema na Mohammed Ali ambao wamejinyakulia Ipod. Wengine ni Bruno Mulokozi pamoja na Edwin Kajuna ambao wameshinda simu za mkononi mpya za nokia 6300.


Christopher Damian 'fundi kinyozi' akionyesha mapesa yake aliyolamba toka Tigo...

Tuesday, March 10, 2009

MWINYI ASISITIZA UPENDO NA AMANI...

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka waumini wa dini zote hususan waislamu na wakristo nchini kudumisha upenda na amani ili kuendelea kuwa na taifa la amani duniani.

Mwinyi alisema hayo wakati wa sherehe za mkesha wa sikukuu ya Maulid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

"Niseme tu, tuendeleze upendo, amani na mshikamano miongoni kwa waumini wa dini zote nchini." Alisema.

Sherehe za mkesha wa sikukuu ya Maulid zilifanyika usiku wa kuamkoa leo katika Viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam na kuhudhuruiwa na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam, akiwemo Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban Bin Simba, Kaimu Mufti Suleyman Gorogosi, Sharif Hussein Badawiy, pamoja na masheikh wakuu toka mikoa mbalimbali.

PICHA ZA MKESHA WA MAULID, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA...


Madrasatul Hidaya katika dufu...


Waumini wamehamasika na dufu wallaah!


Sheikh Mwinyi na Sheikh Gorogosi katika tabasamu...


Sheikh Mohammed Kisenga wa Handeni Tanga akisoma mlango wa 4 kwa mbwembwe...


Kila mtu na pozi lake, mradi burudani... we acha tu!

MANYEMA FC YASHINDA, YAPANDA DARAJA...

Timu ya soka ya Manyema, Manyema FC leo imepanda daraja baada ya kuichapa Mwanza United kwa mabao 2-0 katika mechi ya ligi daraja la kwanza, katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Manyema pamoja na timu nyingine zilizopanda daraja zitashiriki michuano ya Ligi kuu ya Tanzania msimu ujao huku Mwanza United ikiendelea kusotea daraja hilo hilo.


Baadhi ya washabiki na wachezaji wa timu ya Manyema FC wakishangilia...

SAMAKI WALIOIBWA WAANZA KUPAKULIWA...



Picha zote:
Wafanyakazi katika bandari ya ar Des Salaam wakipakua samaki toka ndani ya Meli ya Al Tawariq 1, iliyokamatwa hivi karibuni ikivua samaki isivyo halali.

Monday, March 9, 2009

TNBC KUJADILI MTIKISIKO WA UCHUMI WA DUNIA...

BARAZA la Taifa la Biashara (TNBC), limeandaa mikutano miwili itakayowashirikisha wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa, kujadili namna ya kuchukua tahadhari ili Tanzania isiathirike na mgogoro wa uchumi unaoendelea duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dustan Mrutu, alisema pamoja na kwamba bado Tanzania haijaathirika na mtikisiko huo, lakini dalili zinaonyesha kuwa nayo itaathirika hasa katika upande wa uchumi, biashara na chakula.

“Mtikisiko huu wa kiuchumi umeathiri sana uchumi wa nchi zilizoendelea hali ambayo pia inahatarisha uchumi wetu kwani mazao yetu kama pamba, kahawa na korosho soko litapungua,” alisema.
-Halima Mlacha-


Katibu Mtendaji wa TNBC, Dunstan Mrutu..

WAKILI ATUHUMIWA KUIIBIA BARCLAYS

POLISI Jijini Dar es Salaam inamshikilia mwanasheria wa kujitegemea Theonest Rutashoborwa (44) kwaajili ya mahojiano kuhusiana na tuhuma za kuiibia benki ya Barclays.

Rutashoborwa ambaye anatoka katika kampuni ya wanasheria ya Briliance Law Chamber, anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tuhuma za kula njama ,kughushi na kuiibia benki ya Barclays Dola za Kimarekani 1,081,263.

Alisema mwanasheria huyo anahojiwa kama mtu mwingine anavyohojiwa hivyo endapo atadhibitika kula njama, kughushi kwa aina yoyote ile ataungwanishwa na washtakiwa wengine ambao tayari wameshafikishwa mahakamani kuhusuana na tuhuma hizo.

“Kesi inapofika mahakamani si kwamba uchunguzi wake hauendelei hivyo tunafanya mahojiano na Rutashoborwa ili kubaini kama amehusika na tuhuma hizo au la , endapo atabainika kuhusika sheria itachukua mkondo wake na kama hakuhusika basi lakini si kwasababu ni mwanasheria hawezi kuhojiwa la bali polisi inafanya mahojiano na mtu yoyote yule”.

BOSI WA IMF AMWAGA MAPESA USWAHILINI...


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Dominique Strauss-Kahn akijiandaa kumpatia fedha mmoja wa wafanyabiashara wa chandarua katika soko la Manzese baada ya kununua bidhaa hiyo, leo. Mbali na hapo pia alitembelea katika hospitali ya CCBRT na kuchangia Shs Milioni 6.6. Strauss-Khan yupo nchini kuhudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya sera za shirika hilo kwa Afrika unaofanyika Dar es Salaam kuanzia leo.

MBWA WA POLISI WAPEWA MAFUNZO MAALUMU..


Polisi wa kikosi cha madwa wakiwa na mbwa wawili waliopata mafunzo ya kuguyndua madwa ya kulevya, leo jijini Dar

Uhuru endorsed for presidency in 2012

Kanu chairman Uhuru Kenyatta’s political star received a major boost on Saturday when 14 MPs from across the political divide endorsed him as Central Kenya leader, and for the presidency in 2012.

Mr Kenyatta marshalled the support of the MPs during a fund-raiser in aid of Kimunyu Secondary School in his Gatundu constituency as the fight over the control of the larger Mt Kenya region votes moved a notch higher.

Apart from Mr Kenyatta who is the Finance minister, Internal Security minister George Saitoti (PNU chairman) and Justice, Constitutional Affairs and National Cohesion minister Martha Karua (Narc Kenya leader) and Vice-President Kalonzo Musyoka are also fighting for the region’s support in their bid for the top post.


KANU National Chairman and Deputy Prime Minister Uhuru Kenyatta dances during the KANU National Delegates Conference.