Wednesday, March 4, 2009

Matumaini ya Rashid Lema kurejea mahakamani yafifia...

Mshitakiwa wa 11, katika kesi ya kina zombe na wenzie ya mauaji dhidi ya wafanyabiashara wa madini, Rashid Lema yupo mahututi.

Lema ambaye alilazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakati kesi ikiendelea kwa sasa hali yake inazidi kukatisha tamaa kutokana na baadhi ya ndugu kutoruhusu watu sasa kwenda kumjulia hali wodini, hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika toka kwa mmoja wa mashuhuda, zimesema kuwa kwa sasa hakuna matumaini tena ya Lema kurejea katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo yake kama ilivyofanyika kwa wenzake.

"Hali yake si nzuri ukilinganisha na mwanzo." Kilisema chanzo hicho toka hospitalini hapo leo.

Awali kulienea kwa taarifa kuhusu kufariki kwa mshitakiwa huyo, jambo lililovuta hisia za wengi wakiwamo waandishi wa habari na kuamua kufanyia 'follow up' (kufuatilia) taarifa hizo hospitali ya Muhimbili, leo.


Mmoja wa wasamaria wema akimsaidia Afande Rashid Lema (kulia) kushuka ngazi za mahaka kuu ya Tanzania hivi karibuni wakati kesi yao na kina zombe ilipokuwa ikiendelea..


Taratibu Afande.. enhee... shusha na huo... hewaaa..!

No comments:

Post a Comment