Friday, March 6, 2009

Salma Kikwete akemea ngono zembe kwa wanafunzi wa kike

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete ameitaka jamii ya watanzania hasa wanafunzi wa kike kuacha kufanya ngono zembe ili kuepukana na virusi vya ukimwi.

Mama Salma ametoa wito huo leo mchana wakati wa uzinduzi wa siku ya wanawake duniani, katika viwanja vya mnazi mmoja, Dar es Salaam.

"Ninachowausia, achaneni na ngono zembe, wakati wenu ukifika mtafanya mpaka mtachoka", Alisema Mama Salma.


Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akikata utepe kuzindua siku ya wanawake duniani, viwanja vya mnazi mmoja, Dar es Salaam, leo mchana.

No comments:

Post a Comment