Friday, March 6, 2009

Picha za matukio mbalimbali wakati wa Onyesho la Orijino Komedi


Wananchi wakianza kutawanyika baada ya onyesho kukatishwa kutokana na vurugu kubwa zilizozuka...


Wasamaria wema wakimpatia huduma ya kwanza mtoto Abdulatif Seleman, mwanafunzi wa shule ya Msingi Mnazi Mmoja, mara baada ya kukanyagwa na watu wakati wa onyesho la orijino komedi

Askari wa jiji akimsaidia mtoto Tatu kutembea baada ya kukanyagwa na watu kutokana na vurugu za kuwaona Orijino Komedi


Umati wa watu waliofurika kutazama onyesho la Orijino Komedi wakati wa uzinduzi wa siku ya wanawake duniani

Kundi la Orijino Komedi likishambulia jukwaa wakati wa sherehe za uzinduzi wa siku ya wanawake duniani..

'efu em akademiaaa... wazee wa ngwasumaaa... ale ngwaa.. suu.. maa.. wazee wa ngwasumaaaa...'


Mchekeshaji wa Orijino Komedi akiwasalimia wananchi waliohudhuria onyesho lao wakati wa uzinduzi wa siku ya wanawake duniani..

No comments:

Post a Comment