Friday, March 6, 2009

Orijino Komedi nusura lipoteze uhai wa wanafunzi

Kundi maarufu la vichekesho, Orijino Komedi nusura lisababishe vifo vya washabiki wake kutokana na vurugu kubwa zilizozuka wakati likifanya onyesho lao, katika uzinduzi wa siku ya wanawake duniani, viwanja vya mnazi Mmoja, Dar es Salaam, leo mchana.

Miongoni mwa walionusurika kupoteza maisha ni pamoja na watoto wadogo wanafunzi wa shule za msingi, waliokuwa wakikanyagwa baadhi yao na washabiki waliofurika kuangalia onyesho lao.

Kufuatia vurugu hizo, iliwalazimu kukatisha onyesho hilo na kuondoka zao, hali iliyorudisha hali ya amani kwa washabiki wake.

Watoto Abdulatif Selemani pamoja na Tatu Ally, wanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi mnazi mmoja, ni miongoni mwa walionusurika kupoteza uhai baada ya kuzirai kutokana na wingi wa watu viwanjani hapo.


No comments:

Post a Comment