Thursday, March 5, 2009

Ole wenu Waganga Feki- PINDA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa onyo kali kwa waganga wa kienyeji 'feki' ambao ni miongoni mwa vyanzo vya mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino'.

Waziri Pinda ametoa onyo hilo wakati wa uzinduzi wa zoezi la upigaji kura za maoni kwa wauaji wa walemavu wa ngozi pamoja na vikongwe, katika Viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam jana.

"Nasisitiza tena, serikali yangu ipo makini na waganga watakaogundulika ni feki, ambao ni miongoni mwa wanaotuhumiwa kwa mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi." Alisema.

Uzinduzi wa zoezi hilo umekuja kufuatia vitendo vinavyoendelea vya mauaji ya walemavu wa ngozi pamoja na vikongwe, katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Kwa mujibu wa takwimu za Jeshi la Polisi nchini, vifo vya walemavu wa ngozi kuanzia mwaka 2007 ni jumla ya 43, ambao ni sawa na wastani wa vifo vya walemavu watatu wa ngozi kwa kila mwezi.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo pamoja na viongozi mbalimbali wa ngazi za serikali, wakati wa uzinduzi wa zoezi la upigaji kura za maoni kuhusu mauaji ya vikongwe na albino, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment