Tuesday, March 3, 2009

Matukio mbalimbali ya maombolezo ya marehemu Brig. Jen. Simon Makaranga katika picha...


Baadhi ya maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Meja Jenerali Said Kalembo (katikati) wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Brigedia Jenerali Simon Makaranga, aliefariki dunia mwishoni mwa wiki. Mwili unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kola, Morogoro mjini.


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, Jenerali Davis Mwamunyange akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marahemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Simon Makaranga ( 67), nyumbani kwake Kilakala, mjini Morogoro leo. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kola.


Baadhi ya ndugu wa karibu wa Marahemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Simon Makaranga ( 67) wakiwa katika majonzi nyumbani kwa marehemu Kilakala, Morogoro leo kuomboleza kifo chake kilichotokea mwishoni mwa wiki. Marehemu atazikwa leo katika makaburi ya Kola, mjini Morogoro...

No comments:

Post a Comment