Tuesday, March 17, 2009

TWANGA WATOA MSAADA HOSPITALI MWANANYAMALA..

Uongozi wa Makampuni ya ASET, inayomiliki bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta leo ulifanya ziara katika hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia wagonjwa na watoto waliolazwa hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka amesema ni vema wananchi wakajenga utamaduni wa kutembelea hospitali na kutoa misaada kwa wagonjwa wakiwa ni sehemu ya jamii.

Aidha amezitaka kampuni na wafadhili mbalimbali kuiga mfano wao, kwa kujijengea utamaduni wa kuwasaidia wagonjwa katika hospitali mbalimbali ili kuwapa faraja na ahueni ya kupona haraka ili warejee kuwa pamoja na familia zao pamoja na kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

"Ni wajibu wetu wanajamii kujitokeza na kutoa misaada kwa wagonjwa." Alisema.


Katibu wa bendi ya Twanga Pepeta, Abuu Semhando (wa pili kushoto) akikabidhi moja ya msaada kwa Muuguzi mwandamizi wa hospitali ya Mwananyamala, Angelina Saguti

No comments:

Post a Comment