Thursday, March 5, 2009

Wema Sepetu aachiwa kwa dhamana

Mrembo wa Tanzania (2006), Wema Sepetu ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Kinondoni, Dar es Salaam jana. Mama yake mzazi ndie aliemwekea dhamana Mahakamani hapo.

Awali Wema alikuwa akituhumiwa kuvunja kioo cha gari la msanii wa maigizo na filamu nchini, Steven Kanumba jijini hapa, jambo lililompelekea kuswekwa rumande, kabla ya kufikishwa katika Mahaka hiyo.


Wema akiingia kwenye gari pamoja na mama yake baada ya kuachiwa kwa dhamana, Mahakama ya Kinondoni, Dar es Salaam...


Wema akimkumbatia mchumba wake mara baada ya kutoka Mahakama ya Kinondoni kwa dhamana...



No comments:

Post a Comment